JOKATE ATOA USHAURI UPIGAJI KURA TUZO ZA FILAMU ZA SINEMA ZETU INTERNATIONAL FILM FESTIVAL(SZIFF)

Mlezi wa Tuzo za filamu za Sinema Zetu International Film Festival(SZIFF), Jokate Mwegelo amewashauri watu kutowapigia kura washiriki kwa kuangalia umaarufu walio nao au mahaba walio nao kwao.

Akizungumza leo Desemba 24 katika mkutano na waandishi wa habari, uliolenga kuelezea hatua ambayo mchakato wa tuzo hizo umefika, Jakate ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, amesema watu hawapaswi kuangalia umaarufu kama kweli wanataka kukuza Sanaa hiyo na badala yake waangalie uwezo na kipaji cha mtu.

Amesema kwa kufanya hivyo kutasaidia pia kuja na vipaji vipya badala tasnia hiyo kutawaliwa na watu walewale kila siku na kupongeza hatua ya waandaaji ya kwenda hadi mikoani kusaka washiriki.

“Pamoja na kwamba waandaji wameamua kutoa nafasi kwa watengeza filamu kutoa majina ya wale wanaowaona ni bora katika kipengele cha muigizaji bora wa kike na wa kiume, lakini hii katika upigaji kura haiwazuii kuchagua mnayemuona anafaa, na nina imani hata hao waandaaji hawatatuletea mtu ambaye wanajua hastahili." Amesema

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527