Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi, Humphrey Polepole amesema kuwa katika kipindi mwisho wa mwaka atakuwa katika utekelezaji wa majukumu ya chama bila kupumzika.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa twittwer Polepole ameandika kuwa atakuwa katika mkoa wa Ruvuma akiitekeleza Ilani ya Chama chake chini ya Rais, Dkt. John Magufuli.
"Mwisho wa Mwaka huu niko Mpitimbi, Likuyufusi, Lutapwasi, Mhukuru, Madaba, Bomba Mbili, Mkenda na Lipaya nitakuwa nakagua Utekelezaji wa Ilani ya CCM. Heko John Pombe Joseph Magufuli na Wana CCM kwa kazi nzuri, hongereni", ameandika Polepole.
Akiwa jimboni humo Polepole kwa niaba ya Chama cha Mapinduzi amempongeza Mbunge wa Jimbo la Peramiho, lililopo Wilaya ya Songea Vijijini Mkoani wa Ruvuma, Jenista Mhagama kwa kuekeleza kwa asilimia kubwa Ilani ya chama hicho