BAROKA FC WATWAA UBINGWA SOKA LA USHINDANI AFRIKA KUSINI


Wachezaji wa Baroka FC wakishangilia ubingwa wao.

Klabu ya Baroka FC ya Afrika Kusini, imefanikiwa kutwaa ubingwa wa kwanza wa soka la ushindani nchini humo baada ya kuifunga Orlando Pirates kwenye fainali ya michuano ya Telkom.
Baroka anayochezea mtanzania Abadi Banda imeshinda taji hilo kwa mara ya kwanza baada ya kuifunga Orlando Pirates kwa penati 3-2. Hiyo ilikuwa ni baada ya kutoka sare ya 2-2 kwenye dakika 120.

Baada ya kipigo cha jana Orlando Pirates ambao waliwatoa mahasimu wao Kaizer Chiefs kwenye hatua ya nusu fainali, sasa wameendelea kuwa na ukame wa mataji kwa mwaka wa 4 sasa.

Michuano ya Telkom ilianzisha mwaka 1992 na inashika nafasi ya tatu kwa ukubwa ngazi ya vilabu ikitanguliwa na ligi kuu (PSL) pamoja na ubingwa shirikisho maarufu kaama (Nedbank Cup).

Wakati Baroka FC ambayo inashika nafasi ya 14 kwenye PSL ikitwaa ubingwa wake wa kwanza, Kaizer Chief ndio mabingwa wa historia wa kombe hilo wakiwa wametwaa mara 13.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527