Monday, December 10, 2018

WAKILI HENGA : KURUDISHWA KWA MCHAKATO WA KATIBA MPYA KUTASAIDIA KUPUNGUZA VITENDO VYA UVUNJIFUWA HAKI ZA BINADAMU

  Malunde       Monday, December 10, 2018

Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC ) Anna Henga amesema kuwa, kurejeshwa kwa mchakato wa katiba mpya utasaidia kupunguza vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu.

Kauli hiyo ameitoa mapema leo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika mdahalo maalumu uliowashirikisha viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa pamoja na wadau kutoka asasi mbalimbali za Kiraia.

Amesema bila ya kuwepo kwa katiba mpya na wananchi kupiga kelele katika kupinga uvunjifu wa haki za binadam, matukio hayo hayawezi kupungua na itakua ngumu kuweza kupata uhuru wa kujieleza, hivyo ni vyema wananchi wakaendelea kutetea kurudisha kwa mchakato wa katiba mpya.

Kwa upande wake, Profesa Mwesiga Baregu amesema, vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu umeongezeka kwa kasi kubwa kutokana na vijana kuwa na hofu ya kupigania haki yao.

"Vijana wanatakiwa kuchukua hatua ili kuweza kuleta mabadiliko katika kutetea haki za binaadam katika nyanja zote ikiwemo siasa, uchumi pamoja na kupinga vitendo vya ukatili vinavyoendelea nchini " ,amesema Prof Baregu. 

Ameongeza kuwa, changamoto kubwa inavyokwamisha upatikanaji wa haki za binadamu katika nyanja zote ni uwoga iliyotawala katika nafsi za watu jambo ambalo linahitaji kupingwa kwa njia zote.

Naye, Mbunge wa Kigoma Mjini ambae pia kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe amewataka vijana kuchukua hatua badala ya kulalamika, hivyo ni lazima wachukue hatua mbadala katika masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo.

Amesema  vijana wa zamani walikuwa na umoja katika katika kupigania uhuru wa kuleta maendeleo lakini vijana wa sasa hivi wamekuwa na hofu na wamekosa kujitoa katika kupigania haki zote.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post