BASATA WAMPONGEZA DIAMOND PLATNUMZ..WASISITIZA 'SANAA NI KAZI'

Baraza la sanaa Taifa (BASATA) limechukua uamuzi wa kumpongeza msanii wa muziki nchini Tanzania Naseeb Abduly alimaarufa Diamond Platnumz kwa kuonyesha moyo wake wa kujitolea. 

Baraza hilo limetumia ukurasa wake wa Instagram kuandika ujumbe kwa msanii Diamond na kuchukua nafasi hiyo kuwaomba wasanii wengine kuiga mfano wa Diamond kuweza kuwa msaada katika jamii inayowazunguka.

“Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), linampongeza msanii Nasibu Abdul maarufu kama ‘Diamond Platnumz’ kwa moyo wa kizalendo aliouonesha wa kujitolea shilingi milioni 68 kumalizia ujenzi wa shule iliyopo Wilayani Sumbawanga.

"Kitendo hiki kinazidi kuishawishi jamii kuithamini, kuilinda na kuipenda sanaa yetu nchini. Aidha Baraza linapenda kutumia nafasi hii kuwasihi wasanii wengine nchini kuiga moyo huu ili tuweze kuisaidia jamii yetu inayotuzunguka. SANAA NI KAZI, TUIPENDE NA KUITHAMINI.#HongeraDiamondPlatnumz” -Wameandika BASATA

Hatua hii imekuja baada ya akaunti ya Ikulu Mawasiliano kumpogeza msanii huyo kwa kuamua kujitolea kujenga shule ambayo ilipewa jina lake la Diamond Platnumz Shule ya Msingi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post