Shirikisho la soka Afrika CAF jana Desemba 20 2018 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam limeichezesha droo ya kupanga makundi ya michuano ya mataifa ya Africa kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17.
Michuano ya AFCON U-17 ambayo yatafanyika jijini Dar Es Salaam April 14-28 2019 jini Dar es Salaam itashirikisha jumla ya timu nane ambazo ni Nigeria, Angola, Senegal, Guinea, Uganda, Morocco, Cameroon na Tanzania ambaye ni mwenyeji.