MBUNGE MABULA ACHANGIA MILIONI 22 UJENZI SOKO LA MLANGO MMOJA


Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula (katikati), akizungumza na wafanyabiashara wadogo (machinga) katika Soko la Mlango Mmoja Jijini Mwanza.
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza, Stanslaus Mabula (CCM) ametoa shilingi Milioni 22 kwa ajili ya ujenzi wa sehemu ya soko la Mlango Mmoja iliyoteketea kwa moto miezi mitatu iliyopita.

Mabula aliyasema hayo jana baada ya kuwatembelea wafanyabiashara wadogo (machinga) katika soko hilo na kubainisha kwamba fedha hizo kutoka mfuko wa jimbo zitasaidia
ujenzi wa paa lote.

Mwenyekiti wa soko hilo, Jackson Kayoza alisema kulingana na tathmini iliyofanyika, shilingi Milioni 98 zinahitaji kwa ajili ya ujenzi wa sehemu iliyoungua moto hivyo alimshukru mbunge Mabula kwa mchango huo.

Mmoja wa machinga katika Soko la Mlango Mmoja ambaye pia bidhaa zake zilitekeketea kwa moto, Isaack Julius, alisema mchango wa mbunge Mabula uwe chachu kwa Halmashauri
ya Jiji la Mwanza kwa kuhakikisha inakamilisha kiasi cha fedha kinachohitajika ili ujenzi huo uanze mara moja.

Septemba 28, 2018 majira ya alfajiri, ajali ya moto ilizuka katika Soko la Mlango Mmoja na kusababisha meza 83 za wajasiriamali, maduka 23 na vyoo vitatu kuteketea ambapo hasara yake haikujulikana mara moja.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527