DIAMOND NA RAYVANNY WAIANGUKIA BASATA.. WAKIRI KOSA KUPIGA WIMBO WA NYEGEZI

Wasanii nyota wa muziki nchini Tanzania Diamond Platnumz na Rayvanny wameomba msamaha kwa kupiga kibao chao kilichofungiwa katika tamasha lao hivi karibuni.

Wasanii hao wa Bongo Flava walipiga kibao chao kiitwacho Mwanza katika tamasha lao liitwalo Wasafi Festival. 

Kufuatia kukaidi agizo la Basata, nyota hao wawili walifungiwa kwa muda usiofahamika kufanya onesho lolote ndani na nje ya Tanzania.

Asubuhi ya leo wasanii hao wametoa video katika mtandao wa kijamii wa Instagram ya kuomba radhi kwa 'makosa yao'.

"Kwa unyenyekevu mkubwa tunaomba radhi kwa Jamuhuri yetu tukufu ya Muungano wa Tanzania, Wizara ya Habari Sanaa na Michezo, Basata na kila aliyekwazika kwa kuperform (kupiga) wimbo wa Mwanza katika show (onesho) yetu ya Mwanza. Japo tunajitahidi kuwa vijana wa mfano bora katika taifa letu lakini unavyojua binadamu siku zote hauwezi kupatia. Ni kweli tulikosea kwa kuperform mwimbo ambao umefungiwa. Tunaahidi kutorudia tena kosa lilotokea. Lakini pia kwa kutumia kazi za sanaa kuwasihi wasanii wenzetu na mashabiki kuwa mabalozi bora wa tamaduni za Tanzania," amesema diamond katika video hiyo.

Katika maelezo iliyoamabatana na video hiyo, Diamond ameandika: "Ila Utelezapo, ni vyema kulijua Kosa na Kulirekebisha ili kesho na Kesho kutwa lisijirudie....Inshaallah Mwenyez Mungu Atusimamie na kutuongezea Juhudi na Maarifa katika Kazi zetu ili kwa Pamoja tuzidi kuukuza Muziki wetu na Kuendelea Kuiwakilisha vyema na kulipa sifa Nzuri na Heshima Nchi yetu..."


Wakati wakiufungia wimbo huo, Basata walisema kibao hicho "kimebeba maudhui machafu," ambayo ni "ukiukwaji mkubwa wa maadili ya Kitanzania" na kwamba umetumia "maneno yanayohamasisha ngono".

Baraza pia liliwataka "kuuondoa wimbo huo mara moja kwenye mitandao ya kijamii kabla ya kufika saa kumi kamili" siku hiyo, lakini mpaka saa tatu nanusu ya leo asubuhi bado upo You Tube.

Na Jumanne walisema wanafungia wasanii hao kwa kuonesha dharau kwa mamlaka: "Baraza limefikia maamuzi ya kuwafungia rasmi kutokana na wasanii hawa kuendelea kuonyesha dharau na utovu wa nidhamu kwa mamlaka zinazosimamia masuala ya sanaa nchini na uvunjifu wa maadili uliokithiri unaofanywa na waandaaji wa Tamasha la Wasafi 2018, chini ya uongozi wake Diamond Platnumz," ilisema taarifa ya Basata.

Kibali cha tamasha lao pia kimesitishwa "kutokana na ukiukwaji wa sheria, kanuni na taratibu katika uendeshaji wa tamasha hilo hapa nchini."

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527