SSRA YAKANUSHA KUHUSU FAO LA WASTAAFU


Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii SSRA, kupitia Mkurugenzi Mkuu, Irene Isaka, imekanusha malalamiko ya kupunguzwa kwa mafao ya wastaafu kupitia kanuni mpya za mwaka 2018 na kudai kuwa, taratibu zinazotumika ni za mwaka 2014.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam, Irene Isaka amesema changamoto hiyo inasambazwa na wanachama wachache, pia ni jambo ambalo linaweza kuzungumzika na kuongeza kuwa sheria ambayo imepitishwa inalenga kuifanya mifuko hiyo pamoja ili ilete faida kwa wanachama wake.

“Sheria ya kuunganisha mifuko imeleta usawa wa wanachama, kwa viwango wanavyochangia, kupunguza gharama za uendeshaji, jambo lingine ni kuweka uwaniano kati ya wachangiaji na wastaafu, lakini sasa tuna uwiano mzuri, pia sasa hivi hata akifariki mafao yataendelea kwa miaka 3,” amesema Kisaka.

Isaka ameeleza kuwa, haikuwa sahihi kundi dogo kulipwa kwa mkupuo  wa zaidi ya mara tatu ya michango aliyochanga kwa kipindi chote cha ajira yake tofauti na wenzao hivyo, asilimia 25% iliyopunguzwa kwenye mkupuo imewekwa kwenye pensheni ya kila mwezi ambayo imeongezeka kwa asilimia 50%.

“Sheria hii imetatua changamoto, kwa hiyo niwaondoe wasiwasi lengo ni zuri na hata wanaolalamika ni wachache kwa sababu tunawastaafu zaidi ya laki moja kwa hiyo ni sehemu ndogo ya wanachama wenye hofu,” ameongeza.
=
Novemba 22 mwaka huu, Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya alisema  dhamira ya kuunganisha mifuko ya hifadhi ya jamii ilikuwa ni serikali kukwepa madeni inayodaiwa na mifuko ya hifadhi ya jamii ambayo kwa sasa inafikia trilioni 8 kwa sababu waliwekeza kwenye miradi isiyokua na tija.

Chanzo: Eatv

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527