POLISI ANAYEDAIWA KUBAKA MTOTO AKOSA DHAMANA

Ofisa wa Jeshi la polisi mstaafu Mashaka Mdachi (72) amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Morogoro kujibu shitaka la kumbaka na mwanafunzi wa darasa la tano mwenye miaka 13.

Mbele ya hakimu wa mahakama hiyo Elizabert Nyembele, mwanasheria wa Serikali Mary Lundu alidai mshtakiwa alitenda kosa hilo kati ya Januari 2017 na Oktoba 2018 katika nyakati tofauti huko Area Five kata ya Kichangani Manispaa ya Morogoro.

Mwanasheria huyo alidai mahakamani hapo Ijumaa ya Novemba 23, 2018 kuwa mshtakiwa alifanya kitendo hicho huku akijua ni kosa kisheria na kumuathiri kisaikolojia binti huyo.

Alipotakiwa kujibu shitaka hilo mshtakiwa huyo alikana na mahakama Iliahirisha kesi hadi Desemba 6, 2018 itakapotajwa tena wakati polisi wakiendelea na upelelezi wa kesi hiyo na mshtakiwa alipelekwa rumande baada ya kukosa wa kumdhamini.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527