WATEJA WA TBL KUJISHINDIA MAGARI KUPITIA PROMOSHENI MPYA YA 'TBL KUMENOGA, TUKUTANE BAA'


Meneja wa Udhamini na Mawasiliano ya Wateja wa TBL,David Tarimo (kushoto) na Meneja wa Biashara na ukuzaji wa Masoko wa TB Group na ABInBev kanda ya Afrika Mashariki, Edith Bebwa, wakikata utepe wakati wa kuzindua promosheni ya 'TBL kumenoga, Tukutana baa wengine pichani ni mameneja wa chapa za vinywaji vya TBL.
Mameneja kutoka kitengo cha Masoko wa TBL wakipeperusha bendera wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo.
Meneja wa Biashara na ukuzaji wa Masoko wa TB Group na ABInBev kanda ya Afrika Mashariki, Edith Bebwa,akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi huo.
Meneja wa Udhamini na Mawasiliano ya Wateja wa TBL,David Tarimo akifafanua jambo wakati wa uzinduzi,wengine pichani ni Mameneja wa chapa za vinywaji vya TBL

Na Mwandishi Wetu.

Kampuni ya TBL imezindua promosheni mpya inayojulikana kama 'TBL kumenoga ,Tukutana baa’ kwa lengo la kuwashukuru wateja wake na itafanyika kwenye mabaa mbalimbali nchini kote ambapo washiriki wataweza kujishindia zawadi zawadi mbalimbali ikiwemo zawadi kubwa ya gari mpya aina ya Renault KWDI kwa kila mshindi wa droo kubwa ya mwezi na promoheni itafanyika kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia sasa.

Meneja wa Udhamini na Mawasiliano ya Wateja wa TBL,David Tarimo,alisema kuwa kuwa promosheni hii itafanyika kupitia chapa maarufu za bia zinazozalishwa na kampuni ambazo ni Safari Lager, Kilimanjaro Lager, Castle Lite and Balimi Extra Lager

Kwa upande wake,Meneja wa Biashara na ukuzaji wa Masoko wa TB Group na ABInBev kanda ya Afrika Mashariki, Edith Bebwa, alisema mbali na zawadi kubwa ya gari zipo zawadi nyingi za kujishindia kupitia promosheni hii ikiwemo bia za bure.Alisema promosheni itakuwa inafanyika katika mabaa mbalimbali nchini katika siku za mwisho wa wiki ambapo kila sehemu ya promosheni kutakuwepo bendera ya TBL Kumenoga.

Alisema ili kushiriki promosheni hi ya ‘TBL Kumenoga, Tukutane Baa’ anachotakiwa kufanya mteja ni kununua bia tatu za chapa zilizopo kwenye promosheni ambapo watapatiwa kuponi yenye namba ambazo wanapaswa kuzituma kupitia simu zao za mkononi kwenda namba 15451 kwa kutumia mitandao ya simu ya makampuni ya VODACOM, TIGO na AIRTEL.
Wateja wenye mitandao mingine ya simu wanaweza kushiriki promosheni kupitia tovuti ya http://www.tblkumenoga.co.tz

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post