RC GEITA AVUTIWA NA TEKNOLOJIA YA VETA ,UDSM KUSAGA MAWE YA DHAHABU


Mkuu wa mkoa wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel ameeleza kuvutiwa na kuridhishwa na ugunduzi wa teknolojia zilizogunduliwa na Mamlaka ya ufundi stadi nchini maarufu kama VETA na Chuo kikuu cha Dar es salaam(UDSM) ya kusaga mawe ya Dhahabu alivyoshuhudia katika mabanda ya taasisi hizo katika maonyesho ya teknolojia bora ya uchimbaji na uchenjuaji wa dhahabu katika  uwanja wa kalangalala Mjini Geita.

Akizungumza alipotembelea banda la waandishi wa Habari mkoa wa Geita,alisema kuwa amefurahishwa na teknolojia mpya ya mashine iliyogunduliwa na Chuo kikuu cha Dar es salaam ya kusaga mawe bila kutoa kelele kubwa na bila kutoa vumbi wakatiwa usagaji wa mawe ambayo inaruhusu kuchanganya mawe na maji ili kuzuia vumbi.

Alifafanua kuwa mashine hiyo ya kusaga mawe ni rafiki wa mazingira na afya za binadamu kwa sababu mashine hiyo haitoi kelele kama mashine zingine zinazotumika kwa sasa katika kusaga mawe ya Dhahabu.

Mkuu huyo wa mkoa amesema ametembele mabanda ya VETA ,UDSM na mengine mengi na kueleza kuwa ameridhishwa na ushiriki wa makampuni mbalimbali yalivyoshiriki kuonyesha teknolojia mpya na bora katika sekta ya Dhahabu kuanzia utafiti,uchimbaji na uchenjuaji wake.

Aidha alisema amejifunza mengi yeye binafsi na kwamba alikuwa hajui kama Benki kuu ya Tanzani (BOT) kama ina mpango wa kusaidia wachimbaji katika sekta ya madini hasa dhahabu.

Alisema ameelezwa na BOT kuwa wametenga bilioni 500 kukopesha wachimbaji wadogo na kutoa wito kwa wachimbaji hao kufika kwenye mabanda ya taasisi za kifedha ili kupata ufafanuzi wa namna ya kunufaika na mikopo hiyo ili waweze kufanya kazi zao za uchimbaji kwa faida zaidi.

Maonyesho hayo yatafunguliwa rasmi na Naibu waziri wa madini Stanislaus Nyongo Jumatano tarehe 26 Septemba mwaka huu na kwa mujibu wa mkuu wa mkoa Robert Gabriel,Maonyesho hayo yatafungwa na Mheshimiwa Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Tarehe 30 Septemba mwaka huu. 

Na Mutta Robert - Geita.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527