MAKONTENA YA MAKONDA YAKOSA TENA WATEJA

Makontena ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam jana Jumamosi Septemba 15, 2018 yamekosa tena wateja.

Makontena hayo yameshindikana kuuzwa katika mnada uliofanyika jijini Dar es Salaam. Hii inakuwa ni mara ya nne makontena hayo kushindwa kuuzika.

Akizungumza kwenye mnada huo, mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya udalali ya Yono, Scolastica Kevela amesema mnada huo umeendeshwa lakini mnunuzi hajapatikana.

Kevela amesema hadi sasa bei zinazofikiwa na wateja hazijafikia malengo waliyowekewa. Amesema wao kama madalali wataendelea kufanya utafiti wa kuwapata wateja.

Wateja wachache waliokuwa kwenye mnada huo walionekana kutaja bei lakini hakuna hata mmoja aliyefanikiwa kufikia kiwango kilichowekwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527