ATIWA MBARONI KWA KUMUUA MTOTO WA ALIYEWAHI KUWA MKE WAKE


Jeshi la polisi mkoani Mtwara linamshikilia mkazi wa Mkalapa wilayani Masasi kwa tuhuma za mauaji ya mtoto Clara Thomas (2) ambaye ni mtoto wa aliyewahi kuwa mke wake kwa kumkata panga shingoni.

Akizungumza jana Jumamosi Septemba 15 mwaka huu, kamanda wa polisi Mkoa wa Mtwara, Lucas Mkondya amesema tukio hilo lilitokea jana(Ijumaa) katika Kijiji cha Chibwini baada ya mama mzazi wa marehemu kwenda kumtembelea mama wa mtuhumiwa ili kuwasalimia watoto aliowaacha kwa mwanaume huyo.

“Mtuhumiwa amezaa na mama wa marehemu watoto wawili na baada ya hapo wakaachana, lakini huyu mwanamke, alikwenda Msumbiji na kuolewa kisha kumzaa Clara (marehemu),”amesema Mkondya.

Kamanda Mkondya amesema baada ya mama kukaa muda mrefu Msumbiji alifunga safari kuja Masasi kwa ajili ya kuwasalimia watoto nyumbani kwa mkwewe wa zamani.

“Wakati mama wa marehemu anafika nyumbani hapo, (mtuhumiwa) alikuwa shambani lakini alirudi nyumbani baada ya kupata taarifa kuwa mzazi mwenzake amefika kuwasalimu watoto,” amesema Kamanda.

Kamanda Mkondya ameeleza kuwa, wakati Clara anakwenda nyuma ya nyumba kujisaidia, mtuhumiwa alimfuata nyuma na kumkata panga shingoni.

Amesema polisi wanakamilisha upelelezi na utakapokamilika watamfikisha mahakamni.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post