IRENE UWOYA: NIMEAMUA KUTAFUTA MWANAUME WA RIKA LANGU MAANA MLISEMA DOGO JANJA NI MTOTO

Muigizaji wa Bongo movie Irene Uwoya ametoa kauli ambayo imethibitisha kuachana kwake na mume wake staa wa Bongo flevaDogo Janja.


Kwa mwezi sasa kumekuwa na tetesi kuwa Irene Uwoya ameachana na Dogo Janja huku tetesi hizo zikichangiwa na Safari aliyoifanya Uwoya wiki chache zilizopita nchini Dubai ambako ilisemekana alikuwa na mwanaume mwingine.


Ingawa wawili hao walishawahi kukataa tetesi za kuachana Lakini sasa inaonekana kama wameamua kuweka mambo hadharani kwani Uwoya ameandika maneno ambayo yanaashiria kamuacha Dogo Janja.


Kupitia page yake ya instagram, Uwoya ameweka comment kwa shabiki mmoja aliyemhoji Kuhusu Dogo Janja ambapo ameandika kuwa ameamua kumuacha Dogo Janja na kutafuta mwanaume anayeendana naye kiumri.


Irene Uwoya aliandika maneno haya: "Simlisema wenyewe nitafute wa umri wangu yeye bado mdogo? Sasa nimefata ushauri jamani…..au keshakuwa”.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post