DARASA LA SABA KUANZA MTIHANI KESHO

Baraza la Taifa la Mitihani (Necta), limetangaza rasmi kuanza kwa Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE), utakaofanyika kesho Septemba 5 na 6, 2018 nchini nzima.


Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Septemba 4, 2018, kuhusu mtihani huo, Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde amesema jumla ya watahiniwa 960, 202 wamesajiliwa.


Kati ya watahiniwa hao, Dk Msonde amesema wasichana ni 503, 972 sawa na asilimia 52.49 na wavulana ni 456,230 sawa na asilimia 47.51.


Katibu mtendaji huyo amesema watahiniwa wasioona waliosajiliwa ni 90, wasichana 31 na wavulana 59.


Wenye uoni hafifu ambao wanahitaji maandishi makubwa ni 846, wavulana 475 na wasichana 371.


Dk Msonde amesema mtihani huo ni muhimu kwa wanafunzi kwa ajili ya kupima uwezo na uelewa wa wanafunzi katika yale yote waliyojifunza kipindi ha miaka saba.


"Matokeo ya mtihani huu hutumika katika uchaguzi wa wanafunzi wanaojiunga na elimu ya Sekondari, hivyo hatutasita kuchukua hatua kwa yeyote atakayejihusisha na udanganyifu na kuharibu taratibu zilizowekwa," amesema

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527