AZORY GWANDA ASHINDA TUZO YA DAUDI MWANGOSI 2018Mwandishi wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) Azory Gwanda ambaye amepotea katika mazingira ya kutatanisha tangu Novemba 21,2018 na mpaka sasa hajulikani alipo ameshinda tuzo ya Daudi Mwangosi inayotolewa kila mwaka na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC).

Mwenyekiti wa Jopo la Majaji wa Tuzo ya Mwangosi Mwaka 2018, Ndimara Tegambwage amemtangaza Azory Gwanda kuwa mshindi wa tuzo hiyo mwaka 2018,leo Jumanne Septemba 4,2018 wakati wa mkutano mkuu wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa habari Tanzania UTPC unaofanyika katika ukumbi wa Lush Garden Hotel jijini Arusha.

Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Mtanzania Absalom Kibanda amekabidhi tuzo hiyo kwa mke wa Azory Gwanda  (Anna Pinuni) ambaye hajulikani alipo tangu Novemba 21,2017.

Mbali na kukabidhiwa tuzo hiyo,pia amekabidhiwa cheti cha utambuzi pamoja na shilingi milioni 10.


Azory ambaye ni mwandishi wa kujitegemea wa MCL.alikuwa kituo cha kazi Kibiti mkoani Pwani alitoweka katika mazingira tatanishi Novemba mwaka jana na mpaka sasa hajulikani alipo.

Mshindi huyo wa tuzo ambayo ni kumbukumbu ya kifo cha mwandishi wa habari wa kituo cha Channel Ten na mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari ya mkoa wa Iringa, Mwangosi aliyeuwa na polisi wakati akitekeleza majukumu yake ya kikazi, anajinyakulia fedha kiasi cha Sh10 milioni.

Na Kadama Malunde – Malunde1 blog
Kushoto ni Absalom Kibanda akikabidhi tuzo ya Daudi Mwangosi 2018 kwa mke wa Azory Gwanda.Katikati ni rais wa UTPC,Deogratius Nsokolo.
Kushoto ni Absalom Kibanda akikabidhi cheti cha utambuzi kwa mke wa Azory Gwanda
Mwenyekiti wa Jopo la Majaji wa Tuzo ya Mwangosi Mwaka 2018, Ndimara Tegambwage akitangaza mshindi wa tuzo ya Mwangosi 2018
Jopo la Majaji wa Tuzo ya Mwangosi Mwaka 2018

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post