WABUNGE WA CHADEMA WATOKA NJE KUSUSIA KIAPO CHA MBUNGE WA CCM

Wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wametoka ndani ya Ukumbi wa Bunge wakati Mbunge wa Buyungu, Christopher Chiza (CCM), akiapa.


Tukio hilo lilitokea mapema asubuhi leo wakati baadhi ya wabunge hao wakiwa ukumbini tayari kwa kuanza kwa kikao cha bunge lakini walitoka kabla Spika Job Ndugai, hajaingia na kisha kuingia baada ya Chiza kula kiapo cha uaminifu.


Hali hiyo ilisababisha viti vya upande wanaokaa wabunge hao kuonekana vitupu huku wakonekana baadhi ya wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF).


Chiza ameapa leo baada ya kushinda ubunge wa Jimbo la Buyungu baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Kasuku Bilago kufariki dunia.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527