Sunday, August 5, 2018

VIDEO YA NYOKA AKILA NJIWA BARABARANI YAZUA GUMZO MTANDAONI

  Malunde       Sunday, August 5, 2018
Nyoka amerekodiwa akimla njiwa kwenye barabara yenye shughuli nyingi mashariki kwa London.

Dave Fawbert alimuona nyoka huyo huko Leytonstone, mapema Jumamosi.

Shirika linaloshughulika na wanyama RSPCA limemchukua nyoka huyo na linaomba habari kuhusu ni kwa njia gani alipata kufika eneo hilo.
Video ya nyoka akimla njiwa London yasambazwa sana mitandaoni

Bw Fawbert alisema kwa asilimia 100 nyoka alikuwa akimla njiwa huyo na kwamba tayari alikuwa amemla nusu.

Anasema alitaka kumuona nyoka akiwa safarini nchini Tanzania miaka michache iliyopita lakini hakufanikiwa, lakini sasa amemuona. alisema.

Video hiyo kwenye akaunti yake ya Twitter imesambazwa mara 4,000.
Wengine wanamtaja nyoka huyo kuwa chatu.
Chanzo-BBC
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post