Saturday, August 4, 2018

MREMA : WABUNGE WA CCM WANAMCHONGANISHA RAIS NA WANANCHI

  Malunde       Saturday, August 4, 2018
Mwenyekiti wa TLP, Augustino Mrema amemtaka waziri wa mambo ndani, Kangi Lugola kuwachukulia hatua wabunge wanaomchafua Rais John Magufuli.


Amesema kuna vikundi vya wabunge ambao wanatengeneza chokochoko dhidi ya Rais na kwamba hatua zichukuliwe kabla hawajatimiza azma yao mbaya dhidi yake.


Akizungumza na waandishi wa habari jana Agosti 3 katika ofisi za chama hicho zilizopo Magomeni, Dar es Salaam, Mrema amesema wabunge hao ambao baadhi ni wanachama wa CCM wanahatarishausalama wa Rais kwa kumchonganisha na wananchi.


Mrema ambaye alikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani katika serikali ya awamu ya pili amesema anawafahamu wabunge hao licha ya kutowataja majina yao.


Ameahidi kumpa ushirikiano Waziri Lugola endapo atahitaji kwa kuwa anafahamu mambo hayo kiundani.


"Mimi nimewasikiliza wabunge tena wa CCM kwa mfano waliosema Rais amechukua Trilioni 1.5 ni kweli au ni kumchafua? Kwa hiyo kuna hiyo tabia imezuka ya kumzulia Rais maneno ya uongo na ya kumdhoofisha,"alisema.


Alisema vikundi hivyo nimekuwa vikitengeneza "chokochoko" ambazo zinalenga kumchonganisha Rais na wananchi.


"Wabunge hao nawafahamu na niko tayari kuwataja kabla hawajatimiza uovu kama ilivyokuwa kwangu,"amesema.


Alieleza kuwa atakuwa mstari wa mbele kuhakikisha Rais anaheshimiwa na kuungwa mkono kwa sababu kazi aliyonayo ni kubwa.


Pia amemshauri Rais Magufuli kuwa makini na viongozi wake kwa kuwa wengi wanafanya mambo kwa kutafuta ‘kiki’ na huenda wakawa si rafiki katika kazi zake.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post