MWANAMITINDO ‘ZOMBIE BOY’ AFARIKI DUNIA


Rick Genest 'Zombie Boy'.
Mwanamitindo aliyekuwa akiongoza kwa kuwa na 'tattoo' nyingi zaidi za wadudu kwenye mwili wake, Rick Genest 'Zombie Boy' amekutwa amefariki nyumbani kwake baada ya kujirusha kutoka ghorofa ya nne.

Zombie Boy aliyekuwa na umri wa miaka 32 aliwahi kufanya kazi na msanii kutoka Marekani, Lady Gaga, na kutokea kwenye video ya wimbo wake mwaka 2011 uliokwenda kwa jina la 'Born This Way'. Alijizolea umaarufu kwenye wimbo huo kutokana na muonekano wake tofauti uliowashangaza watu wengi.

Taarifa zilizotolewa na Jeshi la Polisi nchini Canada limesema kuwa mwanamitindo huyo amejiua kwa kujirusha ghorofani katika nyumba aliyokuwa akiishi huku kukiwa hakuna taarifa yoyote aliyoacha ya maandishi.
Msanii Lady Gaga kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa 'Twitter' ameandika ujumbe kuhusiana na kifo cha mwanamitindo huyo aliyetokea kwenye video yake ambapo amesema kuwa binadamu ni vizuri ukawa muwazi wakati unapopitia kipindi kigumu kwani kujiua pekee hakusaidii.
“Kujiua kwa rafiki yangu Rick Genest, ‘Zombie kumenifundisha kuwa unapokuwa katika kipindi kigumu cha mpito unatakiwa kuwa muwazi kwa jamii inayokuzunguka ili uweze kusaidiwa hata kimawazo, kifo cha rafiki yetu kitufundishe vijana kuwa wawajibikaji na tuibadili jamii na dhana potofu za ukikosa muelekeo suluhisho lake ni kujiua”, ameandika Lady Gaga.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.