MOTO WAUA WATOTO WAWILI

Watoto wawili wa kike, mmoja wa miaka miwili na mwingine wa miezi 6 wamefariki dunia baada ya nyumba walimokuwa wamelala kuungua moto. 

Ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo Agosti 7 katika katika kijiji cha Rwazi kata ya Kikuku, Kagera.


Chanzo cha moto huo kinaelezwa kuwa ni kibatari kilichokuwa kikiwaka, kuangukia godoro na chandarua.


Taarifa zinaarifu kuwa wakati moto huo unaanza, mama wa watoto hao alikuwa amekwenda kwa jirani kuomba chumvi.


Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Kagera Agustino Ollomi amesema amepokea taarifa hizo na akatoa rai kwa wazazi na jamii kwa ujumla kuchukua tahadhari.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.