UMEME WADAIWA KUUNGUZA NYUMBA SHINYANGA, MJANE NA WATOTO WANUSURIKA KUFA

Elizabeth Mwandu ambaye ni mjane mkazi wa mtaa wa Mlepa Kata ya Ndala mjini Shinyanga amesurika kifo akiwa na watoto wake wawili mara baada ya nyumba wanayoishi kuteketea kwa moto.

 Tukio hilo limetokea jana Jumatatu Agosti 6,2018 majira ya saa moja jioni ambapo mama huyo akiwa na watoto wake hao sebuleni wakiangalia Tv, ghafla umeme ulikatika na ndani ya dakika moja uliporudi ndipo ikatokea hitilafu na moto kuanza kuwaka, na kuteketeza kila kitu ndani vikiwemo vyakula yakiwemo magunia saba ya mahindi na mchele. 

Akielezea tukio leo mama huyo alisema chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme, ambapo ulipokatika na kurudi ndipo wakaona cheche kwenye mita na kisha moto kuanza kuteketeza nyumba, ndipo akaanza kupiga kelele kuomba msaada kwa majirani lakini mali zote zikateketea na moto huo. 

“Nashukuru Mungu mimi pamoja na watoto wangu tumesalimika na kifo hakuna ambaye amedhurika, lakini tumeweza kuteketeza chakula chote mchele magunia matatu, mahindi magunia manne, pamoja na thamani zote zilizokuwemo ndani zikiwamo na nguo, yani hatujafanikiwa kuokoa hata kitu kimoja,”alisema Mwandu. 

“Mimi ni mjane mume wangu alifariki mwaka jana hivyo naishi na watoto wangu tu, mmoja anasoma darasa la nne, mwingine ana miaka miwili , hivyo naiomba serikali inisaidie sina mahali pa kuishi na sasa nimehifadhiwa tu na majirani,”aliongeza. 

Naye Mama mzazi wa mjane huyo anayefahamika kwa jina la Asha Ngassa, alisema tukio hilo la moto limemsikitisha sana, huku akimshukuru Mungu kwa kumuokoa mtoto wake huyo kunusurika na kifo pamoja na wajukuu wake hao wawili. 

Kwa upande wake diwani wa kata ya Ndala William Shayo, alimpatia pole mama huyo pamoja na kumsaidia msaada wa chakula mchele kilo 20 pamoja na shilingi 10,000/= huku akiomba wananchi wapate kumsaidia mama huyo, ikiwamo na kamati ya maafa ya wilaya. 

Aidha ofisa operationi wa majanga ya moto na uokoaji kutoka jeshi la zimamoto mkoani Shinyanga Edward Lukuba alikiri kutokea kwa tukio na kubainisha kuwa bado wanakabiliwa na uhaba wa magari ya kuzimia moto ambapo mkoa mzima kuna magari mawili pekee ambayo nayo yamechakaa, huku uhitaji ni kuwa na magari matano. 

Na Marco Maduhu - Malunde1 blog
TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI
Elizabeth Mwandu akionesha jinsi mali zake zilivyoteketea kwa moto.Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog
Mali za Elizabeth Mwandu zilizoteketea kwa moto.
Sofa likiwa limeteketezwa kwa moto.
Elizabeth Mwandu (mkono) akiwa namama yake mzazi Asha Ngassa akionesha jinsi moto ulivyoteketeza mali zote vikiwamo na vyakula.
Mali za Elizabeth Mwandu zilizoteketea kwa moto
Diwani wa Kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga William Shayo (kushpto) akimfariji Elizabeth Mwandu akiwa na majirani zake.
Diwani wa kata ya Ndala William Shayo akimkabidhi msaada wa chakula Elizabeth William mchele kilo 20
Diwani wa Kata ya Ndala Williamu Shayo akiendelea kumfariji Elizabeth Mwandu (wa kushoto).

Wananchi wa mtaa wa Mlepa wakiendelea kujadili namna ya kumsaidia mwenzao ambaye amepatwa na majanga ya moto na kuteketeza mali zake zote vikiwamo vyakula.
Diwani wa Kata ya Ndala Wiliamu Shayo akimpa pole Mwenyekiti wa mtaa wa Mlepa Simon Thobias juu ya tukio hilo la moto ambalo limempata mwananchi wake.
Diwani wa Kata ya Ndala William Shayo akieleza jambo.
Ofisa operationiwa majanga ya moto na uokoaji kutoka jeshi la Zimamoto mkoani Shinyanga Edward Lukuba akizungumza juu ya tukio hilo la moto na kukiri kuwepo na kubainisha kuwa bado wanakabiliwa na uhaba wa magari ya kuzimia moto, ikiwa katika mkoa mzima kuna magari mawili ambayo nayo yamechakaa, huku uhitaji ni kuwa na magari matano.

Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527