WANACHAMA WA CCM WAANDAMANA KUMKATAA MBUNGE ALIYETOKA CHADEMA

Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Monduli wameandamana kwenye ofisi za chama hicho wakitaka aliyekuwa Mbunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA), Julius Kalanga aliyejiunga na chama hicho kufuata utaratibu ikiwemo hatua za uteuzi wa nafasi ya kugombania ubunge.


Aidha, Wakizungumza katika Ofisi hizo wamesema kuwa wamesikia taarifa za kuteuliwa kwake bila kufuata utaratibu ikiwemo kukaa vikao na wazee wa kimila Malaigwanani ili waweze kumpitisha.


Hata hivyo, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Monduli amesema kuwa hajashiriki kwenye vikao na wazee wa kimila kama inavyodaiwa na baadhi ya wanachama hao na kwamba utaratibu utatumika katika kuwapata wagombea


“Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinataratibu zake, kina katiba, sheria ambazo zote zitafuatwa katika mchakato huu wa kumpata mgombea ubunge wa jimbo hili la Monduli,”amesema mwenyekiti wa chama wilaya ya Monduli, Wilson Lengima
Theme images by rion819. Powered by Blogger.