Monday, August 20, 2018

Dc Jerry Muro Amshukuru Rais Magufuli kwa kutoa Pikipiki kwa Waratibu wa Elimu

  msumbanews       Monday, August 20, 2018

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mh.Jerry Muro akiwa na baadhi ya piki piki alizowakabidhi Waratibu wa elimu katika halmashauri ya wilaya ya Meru

MKUU wa Wilaya Arumeru mkoani Arusha Mh. Jerry Muro amemshukuru Rais Dk.John Magufuli kwa uamuzi wake wa kuendelea kuboresha sekta ya elimu kwa kutoa vitendea kazi kwa lengo la kuboresha sekta hiyo huku akiahidi kusimamia ubora wa elimu.

Dc Muro amesema hayo wakati akikabidhi Pikipiki mpya 18 kwa waratibu wa elimu katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru ambazo zimetolewa na Rais kupitia Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako, ikiwa sehemu ya mkakati wa Serikali ya Awamu ya Tano Chini ya Rais, Dkt. John Pombe Magufuli ya kufuatilia Ubora wa Elimu Nchini.

"Tunashukuru kwa vitendea kazi hivi ambavyo tumepewa na Rais kupitia Waziri wa Elimu.Tunaamini vitendea kazi hivi vitatumika kwa lengo ambalo limekusudiwa.

" Tutahakikisha tunainua kiwango cha ufaulu katika Halmashauri yetu ya Arumeru pamoja na kuinua kiwango cha elimu.Lengo ni kuhakikisha mtoto wa maskini anapata elimu iliyo bora,"amesema.

Amefafanua kuwa kupatikana kwa pikipiki hizo na kisha kuzigawa kwa waratibu wa elimu wilayani huo kunatoa nafasi ya wao kutimizamajukumu yao ya kufuatilia ubora wa elimu katika shule za Halmashauri ya Wilaya ya Arumeru.

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post