Mgombea Ubunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, Timotheo Mzava amepita bila kupingwa kwenye kinyang'anyiro hiki baada ya wagombea wenzake kutoka vyama vya upinzani kushindwa kurejesha fomu.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Korogwe ambaye ndiye msimamizi wa jimbo
hilo, Dk George Nyaronga amethibitisha mgombea huyo wa CCM kupita bila
kupingwa kutokana na kushindwa huko kurejesha fomu kwa muda uliopangwa
kwa wagombea wa CUF, Chadema na ACT Wazalendo.
Jimbo la Korogwe Vijijini linafanya uchaguzi huo mdogo kumpata
muakilishi wao kufuatia kifo cha aliyekua mbunge wao Stephen Ngonyani
maarufu Majimarefu ambaye alifariki Dunia.
Social Plugin