Monday, August 20, 2018

NAIBU WAZIRI WA AFYA "APIGA STOP' UUZWAJI WA VIFAA VYA KUPIMIA UKIMWI KWA WATU BINAFSI TANZANIA

  Malunde       Monday, August 20, 2018


 
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndugulile amepiga marufuku uuzwaji wa vifaa vya kupimia virusi vya Ukimwi kwa watu binafsi.


Naibu waziri huyo amesema hatua hiyo inatokana na sheria za nchi kutoruhusu mtu kujipima mwenyewe.


Hayo ameyasema leo Agosti 20, 2018 katika hafla ya kukabidhiwa cheti cha ubora wa kimataifa (ISO) kwa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).


Ndugulile amesema kwa mujibu wa sheria iliyopo sasa inaruhusu mtu kupimwa virusi vya Ukimwi na mtaalamu au mtoa huduma kutoka kituo cha afya na si vinginevyo.


"Hivi sasa bado tuko katika hatua ya kubadilisha sheria ili tuweze kuruhusu watu kujipima wenyewe lakini hii itakuwa baada ya majaribio yanayofanyika katika baadhi ya maeneo kuonyesha matokeo chanya," amesema Ndugulile


"Kwa hiyo basi naziagiza taasisi zangu kuhakikisha kuwa zinadhibiti uuzwaji holela wa vifaa hivi katika maduka ya dawa kote nchini," ameongeza.
Na Aurea Simtowe,Mwanachi
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post