Friday, August 31, 2018

CCM YAWATOSA WASANII KUSHIRIKI SHUGHULI ZA CHAMA..ITABAKI NA TOT TU

  Malunde       Friday, August 31, 2018
Katibu Mkuu wa CCM Dk Bashiru Ally amesema chama hicho hakitakuwa na bajeti kwa ajili ya wasanii na badala yake watabaki na vikundi vilivyopo ndani ya chama.


Ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Agosti 31, 2018 wakati akifungua mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM) jijini Dodoma.

Dk Bashiru amesema kwa sasa wasanii watakaoshiriki shughuli za chama hicho, watapewa huduma muhimu pekee ikiwemo malazi, chakula na usafiri.


Akifungua mkutano huo, amesema msanii wa Afrika ni mwana mapinduzi, mpambanaji na kwamba mashairi ya wimbo wake ni lazima yawe na hisia zinazowakera na kuwazomea wanyonyaji.


“Yako wapi mashairi hayo, ziko wapi nyimbo hizo, ziko wapi ngoma hizo za kusifu bara letu na kuwakumbusha vijana bara hili liliwahi kutawaliwa,” amesema.


“Ndio maana nimesema ndani ya CCM hatutakuwa na bajeti ya wasanii tena, hakuna tutabaki na TOT tutaimarisha chombo chetu kile kama alama na Vijana Jazz basi. Tukienda Arusha tutawakuta wasanii kule wataimba mashairi, watacheza ngoma.”

Amesema alipopokelewa makao makuu ya chama hicho aliburudishwa na vikundi vya ngoma, kubainisha kuwa si kwamba wasanii wa nyimbo alizoziita za kurukaruka ni wabaya, bali kibaya kwa mtazamo wake ni ujumbe uliomo ndani ya sanaa hiyo.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post