MTOTO WA MIAKA SABA ABAKWA NA BABA YAKE MZAZI


Mtoto wa kike mwenye umri wa miaka saba amelazwa katika hospitali ya kata ya Marimanti nchini Kenya baada ya kunajisiwa na baba yake kabla ya kukimbia.


Akizungumza kutoka hospitali ambako alikuwa amempaleka msichana, mama yake alisema ni bahati mbaya kwamba baba anaweza kumfanyia binti yake kitendo kiovu namna hiyo.

Alisema mumewe alikuja nyumbani jioni na kuanza kugombana juu ya mtoto wao wa mwezi mmoja akisema kuwa hakuwa wake.

Alimwaga chakula ambacho mke wake alikuwa amemtayarishia kabla ya kumshukia kwa mateke na makofi.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.