KANGI LUGOLA ATISHIA KUFUTA MAKANISA,MISIKITI TANZANIA | MALUNDE 1 BLOG

Sunday, July 29, 2018

KANGI LUGOLA ATISHIA KUFUTA MAKANISA,MISIKITI TANZANIA

  Malunde       Sunday, July 29, 2018

Waziri wa Mambo ya Ndani Mh.Kangi Lugola pamoja na Kanisa la Pendekoste la Leganga, Arumeru,mkoani Arusha akikata ndafu aliyopewa na kanisa hilo alipolitembelea leo Jumapili Julai 29,2018 mkoani Arusha. 
***
Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amesema hatasita kufuta makanisa au misikiti inayoshindwa kutatua migogoro ya taasisi hizo.


Ametoa kauli hiyo leo Julai 29, 2018 katika Kanisa la Pentekoste la Leganga, lililopo Arumeru mkoani Arusha.

“Kuanzia sasa, kanisa lolote au msikiti wowote utakaokumbwa na migogoro na kushindwa kuitatua wenyewe; misikiti hiyo, makanisa hayo nitakwenda kuyafuta mara moja,” amesema.

Amesema hatua hiyo inalenga kuhakikisha yanakuwapo makanisa na misikiti inayohubiri amani na utulivu.

Waziri Lugola ameonya askari Polisi wanaowashusha jukwaani masheikh na wachungaji inapofika saa 12:00 jioni, akisema muda huo ukifika waimarishe ulinzi ili waumini wamalize ibada zao vizuri.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post