MZEE MAJUTO : MI MZIMA ...KAMA NIMEWAUDHI MNISAMEHE....KUFA NI LAZIMA TUTAKUFA TU


Mchekeshaji maarufu nchini Tanzania, Amri Athuman a.k.a Mzee Majuto amesema kuwa nyonga ndio tatizo kubwa linalomsumbua kwa sasa jambo ambalo linamfanya ashindwe kufanya kazi zake kama alivyokuwa hapo awali huku akidai endapo zitaachia basi ataweza kukimbia kama Ronaldo.

Mzee Majuto amebainisha hayo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha eNewz kutoka EATV baada ya kuwepo tetesi nyingi za hivi karibuni kuzushiwa kuwa amefariki jambo ambalo amesema sio vibaya kwa mtu kufariki lakini sio vizuri kumsambazishia mtu uzushi usiokuwa na faida yoyote.

"Nyonga ndio inanisumbua yaani ikiashia tu ikakaa sawa sawa nitaweza kukimbia kama vile Ronaldo. Kutokana na tatizo hili la nyonga nimeshauriwa nifanye mazoezi madogo madogo na sio yale makubwa sana", amesema Majuto.

Pamoja na hayo, Majuto ameendelea kwa kusema "wale wote ambao wananiombea mabaya mimi siwezi kuwalaumu kwasababu Mwenyezi Mungu ametuumba katika hali tofauti lakini ninaomba kama nimewaudhi mimi basi mnisamehe nami pia nimewasamehe lakini mimi mzima sijafa ila nataka niwaambie tu kuwa kufa ni lazima hivyo tutakufa tu".

Mtazame hapa chini Mzee Majuto akifunguka mengine zaidi kuhusiana na kuacha sanaa ya maigizo pamoja na kusamehe pesa zote ambazo anazodai watu.
Chanzo- EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527