Friday, June 29, 2018

SPIKA NDUGAI AKIRI WABUNGE WAMECHOKA KWELI KWELI

  Malunde       Friday, June 29, 2018

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amekiri kuwa wabunge wake wamechoka kweli kweli kuendelea kuwepo katika Jijini Dodoma baada ya kuwepo hapo wakitekeleza majukumu yao kwa takribani miezi mitatu.

Spika Ndugai ametoa kauli hiyo mapema leo baada ya Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa kumaliza kutoa hoja ya kuahirisha Bunge na kushangiliwa kwa kishindo na wabunge waliokuwepo kwenye kikao hicho cha 61 Mkutano wa 11.

Waziri Mkuu ameahirisha shughuli za bunge mpaka Septemba 04, 2018.

Spika Ndugai amesema "Katika hoja zote, hoja ya Waziri Mkuu ndiyo hoja ambayo inaonekana imeunga mkono kwa kishindo. Wabunge walikuwa wamechoka kweli kweli kukaa Dodoma. Hata hivyo Waziri Mkuu tunakushukuru kwa ku - 'Summarize' yale yote ambayo yaliyokuwa yakijadiliwa bungeni".

Pamoja na hayo Spika Ndugai amewashauri Wabunge pamoja na Mawaziri kuwa maoni na michango iliyotolewa kwa kipindi chote cha Bunge yanapatika kwenye 'Hansard' hivyo wanaweza kuitumia ili kupata kumbukumbu muhimu, vikao vya toka harakati za kutafuta uhuru vinapatikana huko ambapo ametaka idara hiyo izidi kuboreshwa.

"Katibu naomba idara ya 'hansard' iweze kuendelea kuboreshwa maana hii ni kumbukumbu muhimu kwa taifa letu. Ukitaka kuyajua mambo mengi yaliyofanyika katika nchi yetu wapi tumetoka na wapi tunapokwenda na hata kiswahili gani kilikuwa kikitumika. Mawaziri mnaweza kuangalia huko" Spika Ndugai.

Chanzo- EATV
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post