Monday, May 21, 2018

JINSI BUNGE LILIVYOLIPUKA KWA FURAHA SUGU ALIVYOINGIA BUNGENI

  Malunde       Monday, May 21, 2018
Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi maarufu Sugu, ameingia bungeni kwa mara ya kwanza leo Mei 21, 2018 tangu aachiwe kwa msamaha wa Rais John Magufuli, Mei 10 mwaka huu.


Baada ya kuingia bungeni, wabunge wa upinzani walilipuka kwa furaha wakimshangilia huku wakigonga meza zao kwa takriban dakika mbili, hali iliyosimamisha shughuli za Bunge kwa muda.


Sugu ameingia ukumbini saa 3:20 asubuhi akiwa ameambatana na mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Kunti Yusuph ambaye alisikika akisema: "Leo bungeni ni Sugu tu."


Wakati anaingia, naibu waziri wa Tamisemi, Josephat Kandege alikuwa anajibu maswali ya wabunge, lakini akalazimika kunyamaza kwanza.


Sugu alikwenda moja kwa moja kwa mbunge wa Mtama, Nape Nnauye na kumpa mkono kisha kwa waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Kazi na Watu wenye Ulemavu, Jenister Mhagama na kumpa mkono.


Alielekea kwa mwanasheria mkuu wa Serikali, Dk Adelardus Kilangi na waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), George Mkuchika akawapa mikopo.


Baada ya hapo akarudi upande wake wa upinzani na kukumbatiana na mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini na kwenda kukaa sehemu yake karibu na mbunge wa Tarime Mjini (Chadema), Esther Matiko.


Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Change aliwaomba wabunge kutulia ili shughuli za Bunge ziendelee, huku akiwatishia kuwa hatawapa nafasi ya kuuliza maswali ya nyongeza.


“Imetosha sasa, imetosha, haya endelea,” alisema Chenge
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post