Monday, May 21, 2018

MWANAMKE AKATWA KOROMEO KWA PANGA NA MMEWE

  Malunde       Monday, May 21, 2018

Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Mary Miyombo (32), mkazi wa Kata ya Hombolo, Bwawani mkoani Dodoma amenusurika kufa baada ya kukatwa koromeo na mumewe wake aliyejulikana kwa jina la Mgowela Anderson.


Chanzo cha kisa hicho kilichotokea Mei 16, mwaka huu kinaelezwa ni wivu wa kimapenzi ambapo inadaiwa mwanamke huyo alikutwa na mwanamume mwingine ndipo mumewe akamjeruhi kwa kumkata na panga kwenye koromeo na kukimbia.


Akizungumza kwa tabu huku akilia, Mary ambaye kwa sasa amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma amesema siku ya tukio akiwa ametoka kuuza pombe kilabuni kijijini hapo alifika nyumbani kwake na kwenda anapoweka fedha zake ambapo aligundua 1,000 haipo jambo lililosababisha kumuuliza mume wake huyo.


“Nilipomuuliza tu kama amechukua hiyo hela ndipo kipigo kilipoanza hadi kufikia hatua ya kunikata na panga shingoni, yaani simtaki tena yule mwanamume kwani hii ni mara ya tatu ananipiga na kunijeruhi na nimekuwa nikimsamehe lakini kwa hili simtaki tena,” amesema Mary.


Mganga Mfawidhi wa hiyo, Caroline Damian amethibitisha kumpokea mgonjwa huyo hospitalini ambaye alilazwa wodi namba 10 na tayari amesharuhusiwa.


Hata hivyo, Kamanda wa polisi Mkoani Dodoma Gilles Muroto alipotafutwa kuzungumzia tukio hilo hakupatikana.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post