ALIYEKUWA NAIBU MEYA CHADEMA ATUMBULIWA

Katibu wa Chadema, Kanda ya Iringa Mjini, Suzana Mgonokulima, ametangaza kumvua uanachama aliyekuwa diwani wa chama hicho, Kata ya Gangilonga, Dady Igogo. Igogo pia alikuwa Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa.


Katika taarifa iliyotolewa leo Aprili 28,2018 imeelezwa kuwa Igogo amevuliwa uanachama kwa kuwa alikisaliti chama kwa kujivua nafasi ya unaibu meya na baadaye udiwani.


“Ndugu Igogo kwa muda mrefu amekuwa na mwenendo usioendana na itikadi, falsafa, madhumuni, kanuni, maadili na sera za chama,” imesema taarifa hiyo.


Taarifa hiyo imesema kamati tendaji ya jimbo katika kikao chake cha dharura kilichoketi Aprili 24 mwaka huu kiliadhimia Igogo avuliwe ujumbe wa kamati tendaji ya jimbo, kwa kwenda kinyume na katiba ya chama kanuni na maadili.


Taarifa hiyo imeeleza kuwa Igogo amevuliwa uanachama kuanzia leo Aprili 28 kama ilivyokubaliwa na wajumbe wa kamati.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527