MAVUNDE AAGIZA KUFIKISHWA MAHAKAMANI WAAJIRI 6,907 WALIOSHINDWA KUJISAJILI WCF


SERIKALI imesema haitabadili msimamo wake wa kuwapeleka mahakamani waajiri wote ambao
bado hawajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia
Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde amewaambia waandishi wa habari leo Machi 6, 2018 jijini Dar es Salaam.



Naibu Waziri ametoa tamko hilo wakati wa ziara yake ya kushtukiza aliyoifanya wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, kuwabaini waajiri ambao bado hawajatekelkeza
takwa hilo la Kisheria ikiwa ni pamoja na wale ambao hawateketekelezi inavyopaswa Sheria ya ajira na mahusiano kazini.

Akiwa kwenye kiwanda cha kugandisha barafu cha Boghal kilichoko Chamazi, Naibu Waziri pia aliahgiza kukamatwa mara moja wafanyakazi watatu raia wa kigeni ambao walikutwa hawana vibali vya kufanyia kazi.


“Dar es Salaam kuna jumla ya waajiri 14,484, na kati ya hao, 6,907, tumebaini bado hawajajisajili na nimewaagiza maafisa wa WCF kuwafikisha mahakamani mara moja kuanzia kesho mashtaka dhidi yao yaandaliwe, (leo).”

Aliagiza Naibu Waziri Mavudne ambaye aliyefuatana na Kamaishna wa Kazi Bi. Hilda Kabisa, na Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi,
(WCF), Bi. Rehema Kabongo.

Aidha Naibu Waziri Mavunde, aliagiza wafanyakazi watatu wa kiwanda cha kugandisha barafu cha Bhogal, kilichoko Chamazi nje kidogo ya jiji kukamatwa na polisi na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria kwa kutokuwa na
vibali vya kufanya kazi nchini.

“Nitoe wito kwa waajiri nchini, kwa mujibu wa kifungu cha 9 cha uratibu ajira za wageni, kinaelekeza kuwa hataruhusiwa mgeni yoyote kufanya kazi nchini bila ya kuwa na kibali, na hawa tumewauliza vibali vyao hawakuwa
navyo kwa hivyo nimeagiza wakamatwe na wapelekwe polisi na kisha wafikishe mahakamani”, alisema Mhe. Naibu Waziri Mavunde.

Ziara ya naibu waziri ni muendelezo wa operesheni inayoendelea nchini kote kuwabaini waajiri ambao hawajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, ikiwa ni pamoja na kuwabaini wale ambao hawatekelezi Sheria ya ajira na mahusiano kazini.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji WCF, Bi. Rehema Kabongo, alisema Mfuko umeanza kutekeleza maagizo ya serikali kwa kuwafikisha mahakamani wale wote ambao bado hawajajisajili na Mfuko ambao wanakabiliwa na
adhabu ya kulipa faini isiyopungua shuklingi Milioni 50, (Milioni Hamsini) au kifungo cha miaka mitano jela au vyote kwa pamoja.

“Nitoe wito kwa wafanyakazi, operesheni hii ndio imeanza na kama bado kuna mwajiri ambaye bado hajatekeleza wajibu wake asisubiri kufikishwa mahakamani” ,alisema.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia
Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde(katikati), akizu nguzma jambo wakati alipofanya ziara ya kushtukiza kubaini waajiri ambao bado hawajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), jijini Dar es Salaam Machi 6, 2018. Wakwanza kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko huo, Bi. Rehema Kabongo.
Mhe. Mavunde, na Bi. Rehema wakipitia nyaraka
Raia wa kigeni waliokuwa wafanyakazi wa kiwanda cha kugandisha barafu, wakiwa kwenye gari kupelekwa kituo cha polisi kwa kosa la kufanya kazi nchini bila kibali.
Raia wa kigeni waliokuwa wafanyakazi wa kiwanda cha kugandisha barafu, wakiwa kwenye gari kupelekwa kituo cha polisi kwa kosa la kufanya kazi nchini bila kibali.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, Bi. Laura Kunenge, (kushoto), akizungumza jambo na Kamishna wa Kazi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Bi.Hilda Kabisama.
Afisa Mwajiri kiwanda cha Carmel Concrete cha Mbagala Kizuiani akijieleza kwa Naibu Waziri Mavunde baada ya kubainika kiwanda hicho kinakiuka Sheria ya Kazi na Mahusiano Kazini. kwa kutowalinda wafanyakazi kwa kuwapatia vifaa vya kujihami.Kiwanda hicho kimetozwa faini ya zaidi ya shilingi Milioni 10 kwa kosa hilo na mengineyo.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughhulikia Kazi, Ajira na Vijana, Antony Mavunde, (mwenye suti), akizunhumza jambo wakati alifanya ziara ya kushtukiza kwenye kiwanda cha Carmel Concrete cha Mbagala Kizuiani jijini Dar es Salaam jana (Machi 6, 2018), ili kubaini waajiri ambao bado hawajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), na ambao hawatekelezi Sheria ya ajira na mahusiano kazini. Jumla ya waajiri 6,907 jijini Dar es Salaam, hawajajisajili na Mfuko na watapelekwa mahakamani. 
Mfanyakazi wa kiwanda cha Carmel akilalamika mbele ya Naibu Waziri Mavunde, kuhusu mazingira mabovu ya kufanyia kazi na mishahara midogo kinyume na maelekezo ya serikali 
Naibu Waziri akiumuuliza mfanyakazi huyo wa kiwanda cha kugandisha barafu, ambacho pia kimebainika kufanya shughuli za kuchomelea vyuma, baada ya kumkuta hana viatu vigumu (gumboots)
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughhulikia Kazi, Ajira na Vijana, Antony Mavunde, akizunguzma mbele ya Meneja wa kiwanda cha Carmel Concrete, Nabil Kassim, (kushoto), kuhusu kutowalinda wafanyakazi wake. 
Naibu Waziri akiongozana na Kmaishana wa Kazi, Bi.Hilda Kabisa na maafisa wengine wakati wakiwasili kiwanda cha kugandisha barafu cha Bhogal, huko Mbagala Chamazi.

PICHA ZOTE NA K-VIS BLOG/KHALFAN
SAID

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527