Picha : POLISI SHINYANGA YAKAMATA GARI LENYE MITAMBO YA MINARA YA SIMU ILIYOIBIWA VODACOM


Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limefanikiwa kukamata gari lenye namba za usajili T.243 CVU Toyota Carina mali ya Mayeka Mlenda mkazi wa Kahama likiwa limebeba mali za wizi ikiwemo betri 9 za minara ya mawasiliano ya simu ya kampuni ya Vodacom.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule alisema mali hizo zimekamatwa kupitia operesheni mbalimbali zinazoendelea likihusisha taarifa za kiintelijensia.

Alisema gari hilo lilikamatwa likiwa na betri kubwa 9 za minara ya mawasiliano aina ya North Star,betri moja ya jenereta aina ya Koba N70 na Copper wire Cable mbili zenye urefu wa mita 28 vinavyokadiriwa kuwa na thamani ya shilingi 12,338,000/= mali ya kampuni ya simu ya Vodacom.

Kufuatia tukio hilo watuhumiwa walikimbia na kulitelekeza gari.
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Simon Haule akionesha waandishi wa habari mali za wizi zilizokamatwa na jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga vilivyokuwa kwenye gari pichani ambazo ni betri na waya - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Waandishi wa habari wakiangalia mali za wizi zilizokamatwa na polisi Shinyanga
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Simon Haule akionesha gari lililokamatwa na mali za wizi
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Simon Haule akifungua mlango wa gari lililokamatwa na mali za wizi mali ya kampuni ya mawasiliano ya Vodacom
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527