MUOSHA MAGARI AKATWA MASIKIO YOTE KWA KISU BAADA YA KULAWITI MTOTO WA MIAKA MITATU SHINYANGA



Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule akizungumza na waandishi wa habari leo Disemba 21,2017.-Picha na Kadama Malunde - Malunde1 blog
****
Kijana aliyejulikana kwa jina la Msigala Salum (24) amekatwa masikio yote mawili baada ya kumlawiti mtoto mwenye umri wa miaka mitatu katika eneo la Majengo Mapya kata ya Lubaga manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga.

Tukio hilo limetokea Disemba 20,2017 majira ya saa tatu asubuhi ambapo kijana huyo anayejishughulisha na shughuli ya kuosha magari mkazi wa Ndala alimdanganya mtoto huyo wakati akicheza na wenzake nyumbani kwao.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo waliiambia Malunde1 blog kuwa kutokana na tukio hilo mtuhumiwa alishambuliwa na wananchi kabla ya jeshi la polisi kufika eneo la tukio na kumuokoa.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Alhamis Desemba 21,2017 Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule alisema jeshi hilo linamshikilia Msigala Salum kwa kosa la kulawiti mtoto huyo mwenye umri wa miaka mitatu ambaye tayari amefanyiwa uchunguzi wa kidaktari.

Akielezea zaidi kuhusu tukio kamanda Haule alisema mara baada ya tukio hilo baba mzazi wa mtoto alimkamata mtuhumiwa na kumkata masikio yote mawili kwa kutumia kisu na kukimbia.
Kamanda Simon Haule akizungumza na waandishi wa habari leo - 

Picha na Kadama Malunde – Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527