Wednesday, December 20, 2017

MBUNGE ALIYEJIUZULU CUF NA KUTANGAZA KUGOMBEA KUPITIA CCM ATUKANWA NA WANANCHI

  Malunde       Wednesday, December 20, 2017
Aliyekuwa Mbunge Kinondoni (CUF), Maulid Mtulia ambaye amehamia CCM ametangaza nia ya kugombea tena ubunge katika jimbo hilo kwa tiketi ya chama hicho tawala.


Desemba 2 Mtulia alijiuzulu nafasi ya ubunge, huku akisema amefikia uamuzi huo bila kushawishiwa mtu yeyote na amebaini Serikali ya CCM inafanya kazi kubwa ya kutekeleza Ilani na imefanya vizuri katika mambo mengi ambayo upinzani iliahidi kuyatekeleza.


Baada ya hatua hiyo, chama cha CUF upande wa Profesa Ibrahim Lipumba kilitangaza kuwaomba radhi wapiga kura wa Kinondoni kwa Mtulia kujiuzulu uanachama kisha ubunge.


Lakini jana Jumanne Desemba 19, 2017 kupitia andiko lake mtandaoni, Mtulia amesema atachukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa ndani ya CCM ili agombee tena nafasi hiyo.


"Kwaza, nawasalimu wote na khasa wananchi wenzangu wa jimbo la Kinondoni. Nawapa pole sana kwa maumivu makali mliyoyapata kutokana na uamuzi wangu wa kujiuzulu ubunge wa jimbo letu la Kinondoni kupitia chama cha CUF. Nawahakikishia kwamba bado nawapenda sana na niko tayari kuwatumikia tena kwa lengo la kuleta Maendeleo kwenye jimbo letu" aliandika Mtulia 

Mtulia alitumia nafasi hiyo kutangaza nia yake kutaka kugombea;"Nichukie fursa hii kutangaza nia kwa wanakinondoni wote na Watanzania kwa ujumla kuwa nitachukua form ya kuomba ridhaa kwenye chama changu cha CCM na endapo chama changu kitaridhia basi nitakuja mbele yenu kuomba ridhaa ya kuwatumikia katika nafasi ya ubunge wa jimbo letu Kinondoni" 

Kufuatia ujumbe huo ndipo hapo baadhi ya wananchi walianza kumpa maneno wakionyesha hisia zao juu ya jambo alilofanya na analotaka kulifanya. 

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post