Mazishi ya Aina yake! BIBI HARUSI AVALISHWA SHELA (Gauni ya Harusi) KWENYE MAZISHI!!

Bibi harusi


Sio tukio la kawaida kukutana na mtu kavaa gauni la harusi kwenye mazishi.. Lakini hii ya leo kali kutoka Kenya, kuna hii stori kutoka Kaunti ya Vihiga, unaambiwa mwanamke aliyefiwa na mume wake akalazimishwa kuvaa gauni ambalo anavaa bibi harusi wakati wa kufunga ndoa, alafu safari ya kwenda kwenye mazishi ikaanza.


Mary Akatsa ni kiongozi wa Kanisa la Jerusalem Church of Christ alikuwa akiongoza kila kitu mpaka mazishi yalipoisha, ukicheki kwenye hii video huyo mama anaonekana mkali hivi kama unaenda tofauti na maagizo yake.. wengine wanapigwa mpaka vibao.


Mazishi yalikuwa kama sherehe tu, kama ukiiona hii video unaweza kuhisi labda watu walikuwa kwenye harusi au sherehe nyingine ya kawaida.

 Unaambiwa huu ni utaratibu wa kawaida kabisa kwa waumini wote wa kanisa hilo, ikitokea mwanamke kafiwa na mume wake lazima avae shela la harusi siku ya mazishi ya mume wake.

TAZAMA VIDEO HAPA CHINI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post