ANGALIA PICHA- SHIRIKA LA AGPAHI LAZINDUA JENGO LA HUDUMA ZA TIBA NA MATUNZO KWA WATU WANAOISHI NA VVU NA UKIMWI MAGANZO KISHAPU!!


Katika mwendelezo wa kuzindua majengo kwa kwa ajili ya  Huduma za Tiba na Matunzo kwa watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI na UKIMWI ,Shirika la AGPAHI (Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative) linalojihusisha na mapambano dhidi ya ya Virusi vya UKIMWI na UKIMWI linalofadhiliwa na watu wa Marekani kupitia Shirika la Kimarekani la Center for Disease Control and Prevention(CDC) nchini Tanzania leo limezindua jengo la kisasa kwa ajili ya shughuli hizo katika zahanati ya Maganzo iliyopo wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.

Ufunguzi huo wa jengo umefanywa na kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga,ambaye ni mkuu wa wilaya ya Kishapu Wilson Nkhambaku huku mkurugenzi mtendaji wa AGPAHI Lauren Rugambwa Bwanakunu akishuhudia shughuli za ufunguzi wa jengo hilo la kisasa lenye vyumba vitano( viwili vya waganga,masjala,dawa na nasaha).

Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt Ntuli Kapologwe akizungumza katika zahanati ya Maganzo ambapo alitoa wito kwa wananchi kujitokeza kutumia kituo hicho.Lengo la kujenga jengo hilo lenye vyumba vya kutosha ni kuondoa msongamano wa wateja na kuongeza ubora wa huduma na usiri.
Kulia ni afisa miradi huduma unganishi kwa jamii wa shirika la AGPAHI mkoa wa Shinyanga Cecilia Yona akiwa na afisa miradi msaidizi AGPAHI Dorcus Simba wakiwa eneo la tukio.
Kundi la ngoma ya Makhirikhiri kutoka Bulimba wilayani Kishapu wakitoa burudani.

Muonekano wa jengo la Huduma za Tiba na Matunzo kwa watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI na UKIMWI .Katika zahanati ya Maganzo kuna choo chenye matundu mawili kwa ajili ya wateja na wahudumu wa afya kujisitiri.
Diwani wa kata ya Songwa ilipo zahanati ya Maganzo Hemed Shaban akizungumza katika zahanati hiyo ambapo alilipongeza shirika la AGPAHI kwa kusogeza huduma za afya kwa wananchi.
Meneja miradi shirika la AGPAHI mkoa wa Shinyanga Dkt Gastor Njau akizungumza katika zahanati ya Maganzo,ambapo alisema AGPAHI itaendelea kusaidia jamii ya watanzania kuhusu masuala ya afya

Mkurugenzi mtendaji wa AGPAHI Lauren Rugambwa Bwanakunu akisoma risala wakati wa uzinduzi huo wa jengo ambapo alisema zahanati ya Maganzo ni kati ya vituo 43 vinavyotoa misaada katika huduma za tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na VVU.

Hadi mwezi Machi mwaka huu,zahanati ya maganzo imeweza kuandikisha wateja 1178( wanaume 406 na wanawake 772) kwenye huduma ambapo kati yao 87 ni watoto walio chini ya umri wa miaka 15 sawa na asilimia 7.Kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga,ambaye ni mkuu wa wilaya ya Kishapu Wilson Nkhambaku akizindua/akifungua jengo hilo.Zahanati ya Maganzo imeweza kuwaanzishia dawa wateja wapatao 802( wanaume 293 na wanawake 509) kwenye matunzo kati yao watoto ni 77 ambayo ni sawa na 10%.

Kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga,ambaye ni mkuu wa wilaya ya Kishapu Wilson Nkhambaku akikata utepe.Zahanati ya Maganzo ina kikundi chenye jumla ya watoto 14 na makundi mawili ya WAVIU washauri.
Kulia ni kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga,ambaye ni mkuu wa wilaya ya Kishapu Wilson Nkhambaku akiwa amekaa kwenye sehemu ya  kusubiria huduma katika jengo hilo,sehemu hiyo kuna TV.Kushoto kwake ni kwa mganga mkuu wa zahanati ya Maganzo iliyopo wilayani Kishapu Dkt Sam Phillip,akifuatiwa na diwani wa kata ya Songwa ilipo zahanati ya Maganzo Hemed Shaban
Hapa ni katika chumba cha mganga wa 1,Kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga,ambaye ni mkuu wa wilaya ya Kishapu Wilson Nkhambaku  akipokea maelezo kutoka kwa mganga mkuu wa zahanati ya Maganzo iliyopo wilayani Kishapu Dkt Sam Phillip


Mkurugenzi mtendaji wa AGPAHI Lauren Rugambwa Bwanakunu akisisitiza jambo katika moja vyumba vya jengo hilo

 Kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga,ambaye ni mkuu wa wilaya ya Kishapu Wilson Nkhambaku akiwa ndani ya moja ya vyumba vya jengo hilo akipata maelezo mbalimbali
 Kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga,ambaye ni mkuu wa wilaya ya Kishapu Wilson Nkhambaku akitoa hotuba yake ambapo alilipongeza Shirika la AGPAHI kwa kuwajali watanzania

 Kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga,ambaye ni mkuu wa wilaya ya Kishapu Wilson Nkhambaku akizungumza katika zahanati ya Maganzo wilayani Kishapu
Kulia ni makamu mwenyekiti wa muungano wa watu wanaoishi na VVU wilayani Kishapu(KONGA)Mzee Selestine Zengo Nyalandu akizungumza wakati wa uzinduzi wa jengo hilo ambapo aliitaka jamii kuacha tabia ya kuwanyanyapaa watu wanaoishi na VVU.Aliyeshikilia kipaza sauti na afisa habari na mawasiliano wa wilaya ya Kishapu ndugu John Mlyambate
Mgeni rasmi Kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga,ambaye ni mkuu wa wilaya ya Kishapu Wilson Nkhambaku akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa AGPAHI na viongozi mbalimbali wa wilaya ya Kishapu na mkoa wa Shinyanga

Picha ya kumbukumbu

Picha ya kumbukumbu

Picha ya kumbukumbu

picha ya pamoja

Kulia ni mwandishi wa habari Victor Bariety,katikati mkuu wa wilaya ya Kishapu Wilson Nkhambaku,kushoto ni mkurugenzi wa Malunde1 blog,Kadama Malunde

Picha ya kumbukumbu

Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post