Picha : SAVE THE CHILDREN YAGAWA VITABU VYA HAKI ZA WATOTO,MAADHIMISHO SIKU YA MTOTO WA AFRIKA SHINYANGA

Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga leo Jumanne Juni 19,2018 imeadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika ambayo huadhimishwa kila mwaka Juni 16 huku Shirika la Kimataifa la Save The Children limetumia maadhimisho hayo kugawa vitabu vinavyohusu haki na wajibu wa watoto kwa maslahi chanya.

Maadhimisho hayo yamefanyika katika viwanja vya Sabasaba vilivyopo Kambarage Mjini Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro.

Shirika la Save the Children limegawa vitabu vinavyozungumzia Azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watoto katika lugha rahisi kwa watoto ili kutetea haki na wajibu wa mtoto kwa maslahi chanya lakini pia vitabu vinavyohusu malezi bora kwa watoto.

Akizungumza wakati wa kugawa vitabu hivyo,Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Watoto mkoa wa Shinyanga, Antonio Chuhila alisema vitabu hivyo vitawasaidia kwa kiasi kikubwa watoto kujua wajibu na haki zao ili kukabiliana na vitendo vya kikatili ambavyo wamekuwa wakifanyiwa.

“Vitabu hivi vimeandikwa na kuchapishwa na shirika la Save The Children na vimeandikwa kwa lugha rahisi kabisa kuwezesha watoto kuelewa haki na wajibu wao”,alisema Chuhila.

Kwa Upande wake,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro alilipongeza shirika la Save The Children kwa kugawa vitabu kwa watoto kwani hiyo ni njia ya kuwasaidia watoto kujua haki zao.

“Niwashukuru sana Save The Children kwa kutoa vitabu vigumu sana kutetea haki za watoto kama watoto hawajui haki zao,lakini kama watoto watajua haki zao itakuwa rahisi kuripoti matukio yanayowasibu,hivyo naomba watoto mkasome vitabu hivi ili mjue haki zenu”,alisema Matiro.

Hata hivyo Matiro aliitaka jamii na wadau wote kushirikiana katika kulinda haki za watoto huku akiwaasa watoto kutonyamazia kimya vitendo vya kikatili wanavyofanyiwa.

Maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika katika manispaa ya Shinyanga yametanguliwa na maandamano ya watoto kutoka Viwanja vya Shycom hadi Viwanja vya Sabasaba,kasha Mkuu wa wilaya Josephine Matiro kukagua vibanda ili kujionea shughuli za maendeleo zinazofanywa na watoto. 

Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika mwaka huu ni “Kuelekea uchumi wa viwanda,Tusimuache mtoto nyuma”.

ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI
Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Watoto mkoa wa Shinyanga, Antonio Chuhila akimuonesha Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro vitabu vinavyozungumzia Azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watoto vilivyotolewa na shirika la Save The Children leo wakati wa maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika katika Manispaa ya Shinyanga - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Muonekano wa moja ya vitabu vilivyotolewa na Shirika la Save The Children kwa watoto wa Manispaa ya Shinyanga
Muonekano wa vitabu hivyo
Katibu wa Baraza la Watoto Mkoa wa Shinyanga Victoria Deogratius akimkabidhi vitabu vinavyohusu haki za watoto mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiangalia vitabu vinavyohusu haki za watoto
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza wakati akiangalia vitabu vinavyohusu haki za watoto vilivyotolewa na shirika la Save The Children
Getruda George akigawa vitabu kwa watoto wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika katika manispaa ya Shinyanga.
Getruda George akiendelea kugawa vitabu kwa watoto
Watoto wakisoma vitabu vinavyohusu haki za watoto
Watoto wakionesha vitabu vya haki za watoto
Watoto wakiwa katika viwanja vya Sabasaba wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika katika manispaa ya Shinyanga.
Watoto wakiandamana kutoka Viwanja vya Shycom kuelekea viwanja vya Sabasaba mjini Shinyanga wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika katika manispaa ya Shinyanga.
Watoto wakiwa wameshikilia bango wakati wa maandamano hayo.
Watoto wakiwa wameshikilia bango wakati wa maandamano hayo.
Maandamano yanaendelea..
Watoto wakiendelea kuandamana
Meza kuu wakiwa wamesimama kupokea maandamano ya watoto katika viwanja vya Sabasaba Mjini Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika katika manispaa ya Shinyanga.
Wadau wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza wakati wa maadhimisho hayo.
Watoto wakiwa eneo la tukio
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika katika manispaa ya Shinyanga
Wadau wa haki za watoto wakionesha bidhaa zinazozalishwa na watoto
Watoto wakitoa burudani ya wimbo wakati wa maadhimisho hayo
Fatuma Omary akisoma risala ya watoto
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akitoa zawadi ya madaftari na kalamu kwa watoto/vijana wanaoishi katika mazingira magumu zilizotolewa na wadau wa haki za watoto katika manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akitoa zawadi ya madaftari na kalamu kwa mtoto
Wanafunzi wa Tuseme Klabu kutoka shule ya Sekondari Mwasele wakiimba shairi.
Watoto kutoka baraza la watoto kata ya Kambarage wakionesha mchezo wa igizo kuhusu haki za watoto
Wadau wa haki za watoto wakiwa katika viwanja vya Sabasaba mjini Shinyanga.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527