Picha : MBUNGE LUCY MAYENGA AMWAGA NOTI KWA AKINA MAMA WAJASIRIAMALI SHINYANGA..ATAKA WASIBEZE VIKUNDI


Mbunge wa viti maalumu mkoani Shinyanga Lucy Mayenga (CCM) amewataka akina mama kuacha tabia ya kubeza kujiunga kwenye vikundi vya ujasiriamali ambayo ndiyo chachu ya maendeleo kwao kwa kuwainua kiuchumi.


Mayenga amebainisha hayo leo Aprili 27,2018 alipokutana na kikundi cha ujasiriamali cha akina mama wa Soko la Nguzo Nane mjini Shinyanga kutekeleza ahadi yake ya kuwaunga mkono ya kuwachangia shilingi milioni moja Taslimu(1,000,000/=), ili kuongeza mfuko wao na waweze kukopeshana ili kupanua biashara zao.

Alisema huwa anasikitishwa na baadhi ya akinamama ambao wamekuwa na tabia ya kujiunga katika vikundi na baadae kujitoa kwa sababu mbalimbali na kutoa wito kwao wasiwe waoga kwenye kuthubutu kutafuta maendeleo pamoja na kutobeza vikundi.

“Natoa wito kwa akina mama muache kubeza vikundi, na msiwe waoga kuthubutu kutafuta maendeleo, na kikundi hiki cha wajasiriamali wa Nguzo Nane nakipongeza sana kwa umoja wenu ambao mnaendelea nao, na leo nimekuja kutekeleza ahadi yangu nawapatia hapa hapa Shilingi milioni moja taslimu,”alisema Mayenga huku akitoa pesa hiyo.

“Naomba pia kikundi hiki cha akina mama wa soko la Nguzo Nane mkisajili kikundi chenu, muunde katiba yenu, muwe waaminifu katika pesa, na muendelee kukopeshana ,na mimi sitachoka kuwasaidia nitakuwa na wasiliana na viongozi wenu, endeleeni kufanya kazi ili muinuke kiiuchumi,”aliongeza.

Naye katibu wa kikundi hicho Flora Silvester ,akisoma taarifa alisema walianza Machi 3 mwaka huu kwa kuhamasishwa na mbunge huyo, na walikuwa 103 lakini wengine walijitoa, na hivyo kubakia wanachama hai 84 mpaka sasa kwenye mfuko wao wana jumla ya Shilingi Milioni 2.6 ikijumlishwa na pesa ya mbunge, na wamekuwa wakikopeshana kwa riba nafuu.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Soko hilo la Nguzo Nane Hassan Baruti alimpongeza mbunge huyo kwa kutekeleza ahadi yake, ambapo tayari kulianza kuzuka kwa maneno kwa baadhi ya akina mama hao kuwa wamedanganywa kusaidiwa, na kufikia hatua wengine kujiondoa.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Mbunge wa Viti Maalumu mkoani Shinyanga Lucy Mayenga akizungumza na akina mama wajasiriamali wa Soko la Nguzo Nane mjini Shinyanga, na kuwataka wasiwe waoga katika kuthubutu kwenye utafutaji wa maendeleo, pamoja na kujiunga kwenye vikundi ili kupeana nguvu ya kupanua wigo wa biashara zao kwa kukopeshana sanjari na kuweza kupata mikopo kwa urahisi kupitia fedha za halmashauri za maendeleo ya jamii asilimia tano. Picha zote na Marco Maduhu- Malunde1 blog & Shinyanga News Blog
Mbunge wa Viti Maalumu mkoani Shinyanga Lucy Mayenga akizungumza na akina mama wajasiriamali wa Soko la Nguzo Nane mjini Shinyanga.
Mbunge wa Viti maalumu mkoani Shinyanga Lucy Mayenga akionyesha pesa Taslimu Shilingi Milioni moja( 1,000,000/-) ambayo aliahidi kuwapatia akina mama hao kwa kuwaunga mkono kwenye kikundi chao.
Mbunge wa Viti Maalumu mkoani Shinyanga Lucy Mayenga akimkabidhi pesa hiyo Shilingi Milioni Moja mwenyekiti wa Soko hilo la Nguzo Nane Hassani Baruti kwa ajili ya kuwaunga mkono akina mama hao wajasiriamali.
Katibu wa Umoja wa Wanawake CCM (UWT) Wilaya ya Shinyanga mjini Rhoda John Madaha akimpongeza mbunge huyo kwa kutekeleza ahadi yake, na kuunga juhudi za Rais John Magufuli za kusaidia watu wanyonge kuwainua kiuchumi.
Mwenyekiti wa umoja wa wanawake CCM (UWT) Wilaya ya Shinyanga mjini Shambuu Katambi, akizungumza kwenye hafla hiyo fupi ambapo aliwataka akina mama ambao hawapo kwenye vikundi wajiunge ili wapate kujikwamua kiuchumi kwa kuanzisha biashara za uzalishaji mali.
Diwani wa Viti maalumu manispaa ya Shinyanga Mariam Nyangaka naye akimpongeza mbunge huyo kwa kutekeleza ahadi yake ya kusaidia kikundi hicho cha akina mama wajasiriamali wa soko la Nguzo Nane, na kuwataka waendelee kujituma kufanya kazi ikiwa maendeleo hayaji kwa kukaa nyumbani.
Akina mama wajasiriamali wa soko la Nguzo Nane mjini Shinyanga wakiwa kwenye hafla yao fupi na mbunge huyo Lucy Mayenga ya kutekeleza ahadi yake ya kuwapatia shilingi Milioni moja kwa ajili ya kuwa unga mkono, ahadi aliyoitoa mwezi uliopita.
Akina mama wajasiriamali wa soko la Nguzo Nane mjini Shinyanga wakiendelea kusikiliza Nasaha za mbunge huyo pamoja na viongozi alioambatana nao, juu ya umuhimu wa kujiunga kwenye vikundi na faida ya kujituma kufanya kazi.
Akina mama wakiendelea na kusikiliza yjumbe mbalimbali kutoka kwa mbunge wa Viti maalumu mkoani Shinyanga Lucy Mayenga na kuwaahidi kuendelea kuwasaidia ili wapate kujikwamua kiuchumi kupitia kikundi chao.
Akina mama hao wakiendelea kusikiliza maneno ya faraja na kutakiwa kutobeza kujiunga kwenye vikundi vya ujasiriamali ikiwa umoja ni nguvu na utengano ni dhaifu.
Akina mama wajasiriamali wa Soko la Nguzo Nane mjini Shinyanga wakiendelea kusikiliza nasaha kutoka kwa Mbunge Lucy Mayenga wakati akitekeleza ahadi yake ya kuwapatia Shilingi Milioni Moja ya kuwaunga mkono kwenye kikundi chao.
Katibu wa kikundi hicho Flora Silvester akimshukuru mbunge Lucy Mayenga kwa kutekeleza ahadi yake
Mwenyekiti wa Soko hilo la Nguzo Nane Hassani Baruti akimpongeza mbunge huyo kwa kutekeleza ahadi yake, ambapo tayari kulianza maneno kwa baadhi ya akina mama hao kuwa wamedanganywa kusaidiwa, na kufikia hatua wengine kujiondoa.
Akina mama wajasirimali wa Soko la Nguzo Nane mjini Shinyanga wakimpongeza Mbunge huyo wa Viti maalumu mkoani Shinyanga Lucy Mayenga kwa kuwaunga mkono kwenye kikundi chao kwa kuwapatia fedha hiyo Shilingi Milioni Moja Taslimu.
Akina mama wajasiriamali wa soko la Nguzo Nane mjini Shinyanga wakimkumbatia pia Mwenyekiti wa umoja wa wanawake CCM (UWT) Wilaya ya Shinyanga mjini, Shumbuo Katambi ambaye aliambatana na Mbunge huyo wa Viti Maalumu Lucy Mayenga kutekeleza ahadi yake ya kusaidia akina mama hao kuwa unga mkono kwenye kikundi chao kwa kuwachangia pesa shilingi Milioni Moja.

Picha zote na Marco Maduhu- Malunde1 blog & Shinyanga News Blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527