Live : MAREKANI,UFARANSA NA UINGEREZA ZASHAMBULIA SYRIA


Shambulio Syria
Mataifa ya Marekani, Ufaransa na Uingereza yamefanya mashambulio wakilenga vituo vitatu huko Syria kama adhabu kwa madai kwamba utawala wa Rais Bashar al-Asad, ulitumia silaha za kemikali dhidi ya raia wake.

Taarifa zinasema milio ya milipuko imesikika katika maeneo kadhaa ya miji wa Damascus na Homs.

Katika taarifa yake rais Trump amedai kwamba vituo vilivyolengwa vinahusiana na utafiti wa uhifadhi na utengenezaji wa silaha za kemikali.

Rais Trump ameongeza kusema kwamba Marekani iko tayari kuendeleza mashambulio hayo hadi utawala huo wa Syria utakapokoma kabisa kutumia silaha za kemikali.

Naye rais wa Syria Bashar al-Asaad anasema kuwa mashambulio yaliotekelezwa na Marekani, Uingereza na Ufaransa yamemfanya kuwa jasiri zaidi ya ilivyokuwa awali kukabiliana na wapinzani wake.
Rais Bashar al-Asaad

Katika matamshi ya kwanza tangu shambulio hilo la alfajiri , bwana Asaad pia alimshutumu kwa kupoteza uaminifu .


Mapema rais Trump alisema kuwa mashambulio hayo yalikuwa yakilenga viwanda vya kutengeza silaha za kemikali vinavyolaumiwa kwa shambulio la kemikali kwa raia wanaoishi mjini Douma wiki moja iliopita.

Bwana Trump alisema kuwa Marekani na washirika wake walikuwa wakitumia uwezo wao dhidi ya ubepari na ukatili. Pia alilaumu Urusi kwa kushindwa kuweka ahadi ya kukabiliana na silaha za kemikali nchini Syria.

Silaha zilizotumiwa na Marekani kushambulia Syria

Ramani ya Syria ikionyesha maeneo yalioshambuliwa

Lakini akizungumza baada ya kutekeleza shambulio hilo Trump pia ameilaumu Urusi kwa kutomdhibiti mshirika wake kutotumia silaha hizo kama ilivyoahidi 2013.

Na kufuatia hatua hiyo, rais Putin ameshtumu vikali mashambulizi yaliofanywa dhidi ya Syria - akiyataja kuwa uchokozi mkubwa.

Hata hivyo wizara ya ulinzi ya Urusi inasema kuwa zana za serikali ya Syria za mfumo wa kujikinga zimefanikiwa kudungua makombora yote kumi na mbili yaliyovilenga vituo vya kijeshi vya huko Damascus ingawa hawakutoa ushahidi wowote.
Helikopta zilizokua katika kituo hicho zinasemekana ndizo zilizotumika kufanya shambulio la kemikali huko ngome ya waasi ya Douma.

Helikopta zilizokua katika kituo hicho zinasemekana ndizo zilizotumika kufanya shambulio la kemikali huko ngome ya waasi ya Douma.

Urusi pia imesema vituo vyao vya kijeshi havikuathiriwa na mashambulio yaliofanywa na Marekani ,Ufaransa na Uingereza.

Hatahivyo vyombo vya habari vya serikali ya Syria vinasema kuwa mashambulio hayo kwenye kituo cha utafiti cha Damascus yalisababisha uharibifu mdogo na mashambulizi katika mji wa Homs.

Ripoti zingine zinaashiria kuwa baadhi ya zana na vifaa vya kijeshi kwenye maeneo hayo vilikuwa tayari vimeondoshwa mapema wiki hii kabla ya shambulio hilo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527