BONGO MOVIE KUMSAFIRISHA MZEE MAJUTO KWENDA INDIA KUTIBIWA

Wasanii wa Bongo Movie wakiongozwa na Steve Nyerere kwa Pamoja wamekwenda hospitali aliyolazwa muigizaji mkongwe mzee Majuto kwa lengo la kumuona na kumpa faraja katika kipindi hiki ambapo amelazwa katika hospitali hiyo.


Pamoja na kwenda hapo wamemkuta Mzee Majuto yupo kwenye hali nzuri huku akijitokeza mdau ambaye ni Kampuni ya ASAS aliyejitolea Ticket mbili kwaajili ya Mzee Majuto kwenda kutibiwa India.


Baada ya hapo Msanii Steve Nyerere alizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa'" Ni kweli tumepata ticket mbili za Mzee wetu kwenda kutibiwa India na siku ya kesho tutakamilisha huo utaratibu wote na sisi tunajaliana kwenye shida tuache haya makundi ya ajabu ajabu kama tunataka kutengeneza Industry lazima tukubaliane, wote tuache porojo hazijengi Industry ila zinakandamiza”

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527