RC SHINYANGA AWASILISHA KILIO CHA UMEME KWA WAZIRI


Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu akitoa salamu kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack wakati alipomtembelea Ofisini kwake mapema leo.
 

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akizungumza na Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu na msafara wake, Ofisini kwake mapema leo.
**
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack amewasilisha changamoto ya kukosekana umeme wa uhakika katika baadhi ya maeneo Mkoani hapa kwa Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu (MB)  leo Jumatano Februari 28,2018 , Ofisini kwake mjini Shinyanga.

Mhe. Telack amesema kuwa kwa upande wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga na Mji wa Kahama suala la umeme bado ni changamoto kwani sehemu za pembezoni hakuna umeme wakati ni umbali mdogo kutoka katikati ya mji.

Amemuomba Mhe. Naibu Waziri kuliangalia suala hilo na kumuhakikishia kuwa, iwapo kutakuwa na umeme pembezoni mwa miji hii, Shirika la umeme TANESCO litaongeza mapato yake ya kila mwezi kutokana na kuongezeka kwa matumizi ya umeme, aidha itasaidia kukuza uwekezaji wa shughuli mbalimbali na kuongeza uchumi.

Aidha, Mhe. Telack ameutaka uongozi wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga kuwasikiliza wananchi na kushirikiana na Ofisi yake wakati wowote kwa masuala mbalimbali kwa lengo la kuwasaidia wananchi wa Mkoa wa Shinyanga.

Mhe. Naibu Waziri Subira Mgalu amepita Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kwa lengo la kumsalimia baada ya ziara yake ya kukagua utekelezaji wa miradi ya REA Mkoani hapa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527