RAIS MAGUFULI KUWATUMBUA VIONGOZI WA MIKOA NA WILAYA ZITAKAZOKUMBWA NA NJAA


Rais John Magufuli amesema Serikali haitatoa chakula kwa mkoa utakaokumbwa na baa la njaa na badala yake viongozi wa mkoa huo watawajibishwa.

Ameyasema hayo leo Jumanne, Julai 25 wakati wa ziara yake ya uzinduzi wa barabara na kuongeza kuwa kiongozi ambaye hatahamasisha watu wake kulima hafai kuwa kiongozi.

“Wilaya ikiwa na njaa nitajua wewe mkuu wa mkoa hufai, mkuu wa wilaya hufai. Mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya atakayeshindwa kuwahamasisha watu wake wafanye kazi, hafai kuwa kiongozi,” amesema.

Amewataka wakuu wa mikoa kuwaondoa katika nafasi zao makatibu tarafa ambao hawahamasishi kilimo.

“Ikiwezekana na wewe mkuu wa wilaya au mkoa, kama unakaa kijijini au ni katibu kata onyesha mfano wako wa kazi. Ukiwa diwani, hivyo hivyo, ukiwa mbunge hivyo hivyo. Ndiyo maana ninatimiza wajibu wangu wa kuhamasisha watu, chapa kazi, hapa kazi tu",amesema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527