UMEIPATA HII YA KICHWA CHA BINADAMU ALIYE HAI KUPANDIKIZWA KWA MTU ALIYEKUFA?...SOMA HAPA

December 2017 inatarajiwa kuwa siku ya kihistoria kwenye sekta ya afya na tiba duniani ambapo utafanyika upasuaji wa kupandikiza kichwa kwa mara ya kwanza utakaofanyika mjini London ikihusisha madaktari 150 na itachukua zaidi ya saa 34.

Kwa mujibu wa Daktari atakayeongoza upasuaji huo Dr. Sergio Canavero, upasuaji huo utafanyika kwa mara ya kwanza kwa binadamu ambapo kichwa cha binadamu aliye hai kitapandikizwa kwenye mwili wa mtu aliyekufa na binadamu huyo kuweza kupata mwili mpya.

Madhumuni ya upasuaji huu ni kusaidia watu waliopata magonjwa ya kupooza viungo, watu wenye vilema vya miguu na magonjwa ya uti wa mgongo kupata matumaini mapya ya kuwekewa mwili mwingine. Upasuaji huu unatajwa kugharimu zaidi ya Dollar millioni 30.


Upasuaji utafanywa kwa mara ya kwanza kwa mgonjwa Valery Spiridonov kutoka Urusi ambaye kitaondolewa kichwa chake na kupandikizwa kwenye mwili wa mtu aliyekufa. Valery Spiridonov amejitolea kufanyiwa upasuaji huou kwa sababu ana tatizo la uti wa mgongo liliopelekea mwili wake kupata ugonjwa wa kiharusi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527