Angalia Picha - Waziri wa Mambo ya Ndani Akiwa Eneo Walipouawa Askari Polisi Wanne Dar

Masaa machache baada ya kutokea tukio la askari polisi kuuawa jijini Dar es salaam usiku wa Agosti 23,2016,waziri wa mambo ya ndani Mwigulu Nchemba alifika eneo la tukio.


ASKARI polisi wanne wameuawa na raia wawili wamejeruhiwa kwa kupigwa risasi na majambazi huko Mbagala, Mbande jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.



Inadaiwa kuwa askari hao walikuwa wakibadilishana lindo katika Benki ya CRDB, tawi la Mbagala Mmbande na mara wakaibuka majambazi 7 wakiwa na silaha na kuanza kuwashambulia kwa risasi na baada ya shambulizi hilo waliondoka na silaha moja aina ya SMG kwa pikipiki wakielekea maeneo ya Mvuti. 



Imeelezwa kuwa majambazi hayo hayakuingia ndani ya benki ila gari la polisi (Leyland Ashok) limeharibiwa kwa risasi. 
 Hii ndiyo taarifa Kutoka kwa Waziri wa Mambo ya ndani Mh. Mwigulu Nchemba aliyoitoa usiku wa Agosti 23,2016


"Usiku huu nimefika Mbande - Temeke,eneo lilipofanyika tukio baya la uhalifu wa kutumia silaha ambapo watu/majambazi zaidi ya saba wakiwa na silaha wamevamia eneo la Benki ya CRDB-Mbande na kuua askari 4 waliokuwa wakishuka kwenye gari tayari kwa kupokezana lindo.


Pia wamejeruhi raia wa kawaida wawili,nimewajulia hali zao na wote wanaendelea vizuri.

Hatutaishia kulaani tu tukio hili na matukio mengine kama haya,natoa rai kwa wahusika kujisalimisha.Vilevile wananchi na raia wema tunaomba ushirikiano wenu katika vita hii ya kupambana na wahalifu hawa na wanaotuzunguka kwenye maeneo yetu"

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba akimjulia hali Raia aliyejeruhiwa

Waziri Nchemba na Kamanda Sirro wakiwa eneo la tukio

Gari ya Polisi ikiwa imezagaa Risasi









BOFYA HAPA KUSOMA HABARI KAMILI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527