
Diwani wa kata ya Bwilingi, Mhe. Lawrence Peter
Mkuu wa shule ya sekondari Chalinze, Mwl. Melkisedeck Komba
NA. ELISANTE KINDULU, CHALINZE
Hayo yalibainishwa na Mkuu wa Shule hiyo Mwl. Melkisedeck Komba alipokuwa akisoma taarifa ya shule hiyo katika mahafali ya 18 jana.
Mwl. Komba alieleza kuwa mwaka 2024 shule ilifaulisha daraja la kwanza wanafunzi 22 walioenda kidato cha tano na wengine kwenda vyuo vya kati.
"Mwaka 2025 tulipata division one 16, two 71, three 83 na four 18. Hatukuwa na zero mwaka jana", alisema Mkuu huyo wa shule.
Mkuu huyo wa shule pia Alitumia fursa hiyo kuwashukuru wadau mbalimbali wa elimu kwa kuwapa vyeti maalumu vya kutambua mchango wao, wakiwemo Ally Kassim Shakha, Joshua Mtamani, Love beauty ,Jema Gombela, Tatu Kikwete na wadau wengine wa maendeleo ya elimu walioisaidia shule hiyo kutokana na changamoto mbalimbali.
Aidha mkuu huyo wa shule aliainisha changamoto kadhaa zikiwemo uhaba wa kompyuta, upungufu wa meza na viti, pamoja na bwalo la chakula na mabweni.
Akijibu taarifa hiyo, Diwani wa kata ya Bwilingu Mhe. Lawrence Pete ambaye alimwakilisha Mhe Mbunge wa Chalinze na Waziri wa Menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora Mhe. Ridhiwani Kikwete, alianza kwa kuwapongeza walimu wa shule hiyo kwa kufaulisha wanafunzi wote 288 mwaka jana na kupata mwanafunzi wa daraja 1.7
Aidha .Mhe Diwani aliikabidhi kompuyuta 10 zilizotoka kwa wadau mbalimbali wa elimu wakiwemo kampuni ya Stalink-kampumi dada magic builder, watengenezaji wa vifaa mbalimbali vya ujenzi wa nyumba waliotoa kompyuta 5, Mmiliki wa hoteli ya Amara waliotoa kompyuta 4 na Mdau Salama Abeid (pochi nene) kompyuta 1.
Mhe Diwani alieleza kuwa kutokana na uongozi bora wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ,Mhe. Samia Suluhu Hassan na Mbunge wa jimbo hilo Mhe. Ridhiwani Kikwete pamoja na baraza Zima la madiwani wa halmashauri ya Chalinze, shule ilipokea shilingi milioni 50 mwaka jana toka serikalini kwaajili ya ujenzi wa bweni na mwaka huu shule imetengewa kiasi cha shilingi mil. 40 kumalizia mradi huo wa bweni la wasichana shuleni hapo.
Aidha Mhe Diwani kwa niaba ya Mhe. Mbunge aliahidi kupeleka viti na meza ikiwa sehemu ya fedha za mfuko wa jimbo .
Katika mahafali hiyo jumla ya fedha shilingi 1,110,000 zilipatikana katika harembee. Shilingi 660,000 fedha taslimu na shilingi 450,000 ahadi.






Social Plugin